Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuwajulisha wanachama wa CCM na Umma wa watanzania kuwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, na kwa niaba ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) imefanya uteuzi wa mwisho kwa wana CCM watakagombea na kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi wa Ubunge katika Majimbo ya Singida Kaskazini, Songea Mjini na Longido.
Kamati Kuu baada ya uchambuzi na tathmini ya kina kwa walio omba dhamana na kwa kuzingatia misingi ya maadili, uchapakazi, uwakilishi bora na wenye tija kwa wananchi, imewateua
wafuatao;-
- Ndg. Monko Justine Joseph, Mgombea wa CCM-Jimbo la Singida Kaskazini
- Ndg. Damas Daniel Ndumbaro, Mgombea wa CCM Jimbo la Songea Mjini
- Ndg. Dkt. Stephen Lemomo Kiruswa, Mgombea wa CCM Jimbo la Longido
Chama kinawatakia maandalizi mema ya uchaguzi chini ya Uongozi na uratibu wa Mikoa, Wilaya na Majimbo husika, hii ikijumuisha kuchukua fomu za uteuzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) tarehe 16 Disemba 2017.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na,
HUMPHREY POLEPOLE
KATIBU WA NEC – IT
Comments