Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Ibrahim Class leo amekabidhiwa hundi ya shilingi milioni 18 na Naibu Waziri Sanaa Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza.
Class amekabidhiwa hundi hiyo zikiwa ni fedha zake baada ya kufanikiwa kutetea ubingwa wa Dunia GBC dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika Kusini.
Ilifanyika hafla kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Class amekabidhiwa hundi hiyo mbele ya Waziri wa Wizara hiyo, Dk Harrison Mwakyembe.
Pamoja na Dk Mwakyembe, wadau wengine mbalimbali wa mchezo wa ngumi walijitokeza wakati wa halfa hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Bondia huyo alimeishukuru Serikali na wadhamini ambao walidhamini pambano lake pamoja na Watanzania waliojitekeza siku ya pambano hilo lililofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar
Comments