Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga leo itaikingia kambi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za Klabu Bingwa Afrika na mechi za Ligi zilizosalia.
Kocha Mkuu wa timu hiyo ya jangwani Dar es Salaam, George Lwandamina hivi karibuni alitoa mapumziko ya siku saba kwa wachezaji wake ambapo leo wote wanatakiwa kuripoti kambini isipokuwa wale walioko kwenye majukumu ya kucheza timu ya Taifa Stars.
Kuna michuano ya Kombe la Chalenji ambayo inaendelea nchini Kenya hukubaadhi ya wachezaji wenye majina makubwa wa Yanga wakiwakilisha nchi zao huko.
Lwandamina aliweka wazi hapo kabla kuwa majukumu ya timu ya Taifa hayawezi kuharibu mwenendo wa ratiba zake kwani atalazimika kufanya kazi na wachezaji waliopo.
Yanga inakabiriwa na kibarua cha kutetea ubingwa wa Ligi, michuano ya Kombe la Mapinduzi sambamba na ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Comments