Skip to main content

George Weah, mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais

Makamu wa rais Joseph Boakai akubali kushindwa Liberia

J
media
Makamu wa rais waLiberia Joseph Nyuma Boakai ampongeza George Weah kwa ushindi wake Desemba 29, 2017 katika hotuba alioitoa Monrovia, mji mkuu wa Liberia
Siku moja baada ya tume ya uchaguzi nchini Liberia NEC kumtangaza nyota wa zamani wa Soka, George Weah, mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini humo, makamu wa rais Joseph Nyuma Boakai amekubali kushindwa na kumpongeza mpizani wake.
George Weah alishinda kwa 61.5% ya kura , huku mpinzani wake, Makamu wa rais Joseph Boakai akipata 38.5% , Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza.
Weah atachukua nafasi ya Ellen Johnson Sirleaf ambaye alikuwa rais wa kwanza mwanamke barani Afrika kuchaguliwa kidemokrasia na sasa anatarajiwa kukabidhi madaraka kwa amani.
Rais Sirleaf alimshinda Weah katika uchaguzi wa duru ya pili uliofanyika mwaka 2005, baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo kadhaa nchini humo.
Punde baada ya taarifa za ushindi wa Weah kuanza kuenea, maelfu ya wafuasi wake wamejitokeza kwenye viunga vya miji mbalimbali nchini humo kushangilia ushindi wake, mamia ya watu wameonekana mjini Monrovia wakishangilia.
Mwanasoka huyu wa zamani aliyefanya kampeni zake chini ya muungano wa mabadiliko ya kidemokrasia, aliwashawishi vijana kumpigia kura huku mpinzani wake makamu wa rais Boakai akionekana kama mzee.
Hata hivyo ushindi wa Weah umekuja huku akikabiliwa na ukosolewaji kutokana na kumteua mgombea mwenza wake Jewel Taylor aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa nchi hiyo Charles Taylor anayetumikia kifungo nchini Uingereza kwa makosa ya kivita.
Weah mwenye umri wa miaka 51 alishinda duru ya kwanza ya uchaguzi huu uliofanyika mwezi Octoba kwa asilimia 38.4 ukilinganisha na mpinzani wake aliyepata asilimia 28.8, matokeo ambayo yaliwafanya wagombea wote wawili kwenda kwenye duru ya pili.
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Liberia siku ya Alhamisi ilisema kuwa zaidi ya asilimia 98.1 ya kura zote zimeshahesabiwa na Weah alikuwa anaongoza kwa asilimia 61.5 huku mpinzani wake Boakai akiwa na asilimia 38.5.
Weah amewahi kuvichezea soka vilabu kadhaa barani Ulaya ikiwemo klabu ya AC Milan ya Italia, Chelsea ya Uingereza na PSG ya Ufarana, na amekuwa mchezaji pekee kutoka barani Afrika kushinda taji la mchezaji bora wa dunia inayotolewa na shirikisho la mpira duniani Fifa.
Mwanasoka huyu aliingia kwenye siasa mwaka 2002 baada ya kustaafu soka na kwa sasa alikuwa seneta katika bunge la Liberia.
Nchi ya Liberia iliyojengwa na watumwa weusi wa Kimarekani katika karne ya 19, haijawahi kuwa na mabadilishano ya madaraka ya amani kutoka kwa rais mmoja kwenda mwingine tangu mwaka 1944.
Pingamizi la kisheria lilichelewesha uchaguzi huu wa duru ya pili kwa majuma saba na idadi ya watu waliojitokeza kuoiga kura ilikuwa ndogo ukilinganisha na iole iliyojitokeza kwenye uchaguzi wa mwezi Octoba.
Zaidi ya watu milioni 2 walikuwa wamesajiliwa kupiga kura katika taifa hilo lenye watu milioni 4.6.
Rais Sirleaf alichukua madaraka mwaka 2006 baada ya mtangulizi wake Charles Taylor kulazimishwa kuondoka madarakani na waasi mwaka 2003 na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Taylor anahudumu kifungo chake cha miaka 50 jela nchini Uingereza kwa makosa ya uhalifu wa kivita kwenye mzozo wa nchi jirani ya Sierra Leone.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Uganda Police issue fresh terror alert

  By Chris Kiwawulo, The Police have issued a fresh terror alert against a possible attack on Uganda by four terrorists from Kazakhstan. Police spokesperson Judith Nabakooba “We have received a security notification in form of an orange notice of four terrorists originating from Kazakhstan who are planning to travel to foreign countries in order to commit attacks and participate in hostile acts,” Police spokesperson Judith Nabakooba said in a statement on Monday. Nabakooba named the four active members of radical organizations as; Nassiruauly Kairat, Umurzakov Marat Eskendirovich, Kovtun Denis Valerevich and Mazhibayen Alimzhan Akhlazhanovich. By press time, a search on the international web has not yielded anything on the named persons.Last evening, police said that in collaboration with other security agencies vigilance has been stepped up to avert the terrorists’ evil plans. Police have in the past issu...

Poland’s GROM special services mastermind found dead

Brigadier General Slawomir Petelicki, responsible for the formation of the GROM special services unit in the 1990s, was found dead at his apartment, Saturday, with bullet wounds to the head. SÅ‚awomir Petelicki, 1946-2012. Photo: Archive/PAP/Radek Pietruszka Police spokesman Maciej Karczynski informed that Petelicki’s body was found by his wife in the garage of his Warsaw apartment on Saturday. He was 65. Primary investigations point to suicide as the cause of death. It is expected that prosecutors will decide on an investigation into Petelicki’s death on Monday. After examining the scene of the incident, “the body of General [Petelicki] has been taken to a forensic laboratory, although a post-mortem will probably take place on Monday,” prosecutor Katarzyna Calow-Jaszewska from the Warsaw District Prosecution told the PAP news agency. “He was a tough man, a brilliant soldier and commander,” Colonel Krzysztof Przepiorka, head of the ...