takriban watoto 100 wamekamatwa kufuatia uvamizi wa shule moja inayofunza dini ya Kiislamu nchini Kenya
Baadhi ya wahubiri na takriban watoto 100 wamekamatwa kufuatia uvamizi wa shule moja inayofunza dini ya Kiislamu nchini Kenya kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
Haijulikani ni kwa nini uvamizi huo katika mji wa likoni pwani mwa Kenya ulifanyika .
Hatahivyo ripoti kadhaa zinasema kuwa vikosi vya usalama vya kimataifa vilihusika huku Marekani na Uingereza zikidaiwa kuhusika.
Vyombo vya habari vinahusisha uvamizi huo na eneo moja la kukuza ugaidi mbali na biashara haramu ya kusafirisha watoto inayohusisha mataifa kadhaa na mabara.
Gazeti la The Star liliripoti kwamba watoto hao ni wa hadi umri wa miaka mitano na wanatoka umbali wa Marekani, Uingereza na Canada pamoja na mataifa mengine ya bara Afrika.
Duru moja ya polisi ambayo imekataa kutajwa iliambia chombo cha habari cha Reuters kwamba shule hiyo ya madrassa ilikuwa kituo cha kuwapatia wanafunzi mafundisho ya kuwa na itikadi za wapiganaji na kimekuwa kikichunguzwa kwa mara kadhaa.
Sheikh Hassan Omar, ambaye ni afisa mkuu katika baraza la maimamu na wahubiri nchini Kenya CIPK , amboa ni mwavuli wa viongozi wa kidini nchini Kenya aliambia waandishi kwamba watoto hao walikuwa wakilala wakati kundi la maafisa wa polisi wa kigeni pamoja na wale wa nchini walipovamia.
Kuna takriban wanafunzi 100 na walimu wanne wa madrassa ambao wamekamatwa na kuzuiliwa katika makao makuu ya polisi na hakuna mtu anayesema ni uhalifu gani waliotenda.
Afisa mwandamizi wa polisi aliambia Reuters kwamba watoto hao wataachiliwa huru mmoja baada ya mmoja baada ya kuhojiwa.
Comments