Bondia Mtanzania, Idd Pialali amsema amefurahia wake kufuatia kushinda mkanda wa ubingwa wa kimataifa wa ujulikanao kwa jina la ( UBO) baada ya kumchapa mpinzani wake Shiva ambaye ni raia wa India pointi kwenye Ukumbi wa Travel Lodge ambao pia wanatajwa kuwa wadhamini katika pambano hilo lililofanyika wilayani Bagamoyo mwisho wa wiki iliyopita.
Pialali amliambia gazeti hili jana kuwa pambano hilo lilikuwa kubwa na kuwa ni mara ya kwanza kufanyika Bagamoyo ingawa awali alisha pamana wilayani humo, lilianza kwa mabondia kucheza kwa tahadhari kutokana na kusomana.
Alisemma licha ya kibuka na ushindi huo amedodosa kuwa ameshinda pambano hilo ila lilikwenda nje na mipango yake kwani alikuwa akiitaji ushndi wa mapema zaidi hila mpinzani wake kutoka India alikuwa makini hali iliyomfanya kusogeza zaidi raundi katika mpambano.
"Nilikuwa nimeisha jiandaa miezi michache baada ya kuibuka na ubingwa wa Global Tv, Afrika Mashariki nakati siku chache tu hivyo ilikuwa ni mpango wangu kutaka kumpiga dakika za mapema ila mazoezi ya katika maandali ya npinzani nafikiri yaliweza kumsaidia Shiva,"alisema Pialali.
Pialali alisema kuwa kupitia pambano hilo alisema ushindi huyo ameupata kupitia wadhamini kama Kinite Castle ambao ni wamiliki wa ukumbi mpya iliozinduliwa Desemba 17 Jumapili iliyopita katika mji huo mkongwe wa Bagamoyo.
Kwa mujibu wa Promotor wa ngumi aliyeandaa mpambano huo Sharifu Muksini alisema kuwa pambano hilo lilichangia kuonekana kwa mabondia wengine chipukizi ambapo waliona kukuza vipaji kutazaidia kujenga mvuto kwa kuwapa ushawishi mabondia wa wilayani humo kupata mwamuko katika mchezo wa ngumi.
Mwandaaji huyo wa masumbwi amesema siku zijazo anamtazamo wa kumkutanisha tena Pialali katika pambano litakalo kuwa la ubingwa mkubwa zaidi .
ushindi wa majaji wote watatu dhidi ya mpinzani wake ambapo jaji wa kwanza Laszlo Fejes alitoa pointi kwa 98-90, Agapeter Mnazareth 98-91 na Robert Kasiga 97-93.
Mwishoo
Comments