Watanzania wametakiwa kuitunza na kuithamini misitu ikiwemo kuepuka kuikata hovyo ili kuondokana na changamoto ya ukosefu wa mahitaji muhimu yanayotokana na misitu.
Afisa Misitu wa wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Florian Mkeya ameyaeleza hayo leo wakati akizungumza na chanzo kimoja cha habari jijini Dar es salaam ambapo amesema ni vyema watu wakaiheshimu misitu kwani inasaidia vizazi vya leo na baadae.
Mkeya amesema hakuna mahali ambapo watu hawategemei misitu hivyo watu wanapaswa kuepukana na uharibifu wa ukataji wa misitu na kuchoma mikaa pasipo kufata taratibu za upandaji wa miti.
Amesema misitu inasaidia nyanja mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuendeleza shughuli za utalii unaotokana na mazingira halisia ya misitu.
Afisa Misitu Mkeya amesema kuanzia mwaka 2015 walipata ufadhili kutoka shirika la maendeleo la Dunia la UNDP kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usimamizi wa bayanuai katika mtandao wa misitu 12 ya asilia ili kutangaza vivutio mbalimbali katika sekta ya utalii.
Comments