WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Issack Kamwelwe amesitisha manunuzi yote ya vifaa vya maji yanayofanywa na Bohari Kuu ya Maji
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Issack Kamwelwe, amesitisha manunuzi yote ya vifaa vya maji yanayofanywa na Bohari Kuu ya Maji jijini Dar es Salaam hadi hapo Serikali itakavyoelekeza vinginevyo.
Mhe. Kamwelwe, (kushoto), akionyeshwa moja ya vifaa vya maji vinavyotunzwa kwenye bohari kuu ya maji na Meneja wa Bohari Kuu ya Maji Bw. Clepline Bulamo
ya maji au zinazoendesha utoaji wa huduma ya maji waende bohari kuu kuangalia vifaa vinavyoweza kutumika kwao ili wavinunue viishe kabla ya kuelekea kwenye hatua nyingine.
Kumekuwepo na ununuzi holela wa vifaa Halmashauri na Mamlaka za maji zimekuwa zikijinunulia vifaa jinsi wanavyotaka nah ii ni hatari sana ndio maana miradi mingi haiendani na thamani halisi ya vifaa, na vinapatikana kwa gharama kubwa mnno, Aalisema Mhandisi Kamwelwe.
“Mamlaka zote za maji zilizo chini ya wizara yangu, mtu asije akaenda kununua vifaa nje ya bohari kuu kama kifaa hicho kinapatikana kwenye bohari hiyo.” Alisema Mhandisi Kamwelwe.
Na kumuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwenye bohari hiyo kwani kwa hali ilivyo imeshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake.
Mheshimiwa Waziri alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea bohari hiyo iliyoko Boko jijini Dar es Salaam, mwanzoni mwa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji inayotekelezwa na Serikali kupitia DAWASA Desemba 5, 2017.
Alilaumu utendaji duni wa watendaji wa Bohari hiyo unaoonyesha kuishiwa ubunifu. Na hivyo kufanya shughuli kulegalega.
“Serikali imenunua vifaa vyenye thamani ya shilingi bilioni 4.83 vingine vinaonekana vimepitwa na wakati, lakini vingine vinaonekana vinaweza kutumika, na boharia inahitaji watu ambaom ni wabunifu, na kwa vile vilivyopitwa na wakati viko viwanda vinatengeneza vifaa kama hivyo uongozi ni bora ukawasiliana na viwanda hivyo ili waone tatizo ni nini na inawezekana kuboresha eneo ambalo linavifanya visitumike ili vikaweza kutumika na kuokoa fedha za serikali.
“Nakuagiza ufanye kazi hiyo kwa haraka na umpatie taarifa Katibu Mkuu, sitaki kuona kitu hata kimoja kinapotea kwani vifaa hivi vimenunuliwa na kode za wananchi na fedha za serikali.” Aliagiza Waziri Kamwelwe.
Katika hatua nyingine, Waziri amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, kufanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji kwenye bohari hiyo ili pawepo na wataalamu husika kuloingana na shughuli za bohari.
Aidha Waziri ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wadeni wote wa Bohari Kuu ya Maji, kulipa madeni yao vinbginevyo atachukua hatua baada ya muda huo kupita.
Aidha Waziri ametoa muda wa mwezi mmoja kwa wadeni wote wa Bohari Kuu ya Maji, kulipa madeni yao vinbginevyo atachukua hatua baada ya muda huo kupita.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Issack Kamwelwe, akiangalia dira za kupimia maji, alipotembelea bohari kuu ya maji Boko jijini Dar es Salaam, Desemba 5, 2017.
Comments