Jay Z amesema kuwa pamoja na kwamba amepitia wakati mgumu katika ndoa yake na mrembo Beyonce lakini malumbano ya kwenye mitandao ya kijamii ilisaidia kuweka jina lake juu kibiashara.
Jay Z pia alisema kwamba hapendi bifu lakini ugomvi yake na Beyonce na ule dhidi ya rapa Kanye West vilisaidia kuzidi kuliweka jina lake juu.
“Katika sanaa kuna mambo mengi na wakati mwingine malumbano yetu sisi kwa sisi husababisha majina yetu yaendelee kuwa juu pamoja na kwamba ni vitu ambavyo hatuvipendi kwa sababu vinatuchafua,” alisema rapa huyo.
“Kuna wakati nililazimika kufanya kazi ya muziki na Beyonce ili kuondoa wingu zito lililotanda, lakini jamii haikuweza kunielewa, ilibaki ikiendelea kunihukumu,” aliongeza.
Jay Z alikuwa akituhumiwa kuendekeza michepuko, jambo ambalo lilitaka kuathiri mwenendo wa ndoa yake.
Comments