Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2016

Shule 18 Dar kunufaika na elimu ya usalama barabarani

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. 1404w" alt="Eric Potin" width="702" height="336" class="attachment-main-slider size-main-slider wp-post-image no-display appear" style="display: block; margin-left: auto; margin-right: auto;" title="Shule 18 Dar kunufaika na elimu ya usalama barabarani kutoka kwa CFAO Motors Group na Alliance Autos" /> Katika kusaidia kupambana na ajali za barabarani kwa watoto wa shule za msingi jijini Dar es Salaam, kampuni ya CFAO Motors Group kwa kushirikiana na Alliance Autos ambao ni wauzaji wa magari ya Volkswagen wametoa msaada wa elimu na vifaa vya usalama barabarani kwa shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam. Akizungumzia msaada huo Meneja wa Volkswagen nchini, Tharaia Ahmed amesema kuwa lengo la kutoa elimu na vifaa hivyo ni kuwasaidia wanafunzi wa shule ambao wengi wao

Huyi hapa Mchezaji bora mwezi Januari 2016

Beki Shomari Kapombe wa timu ya Azam FC Beki Shomari Kapombe wa timu ya Azam FC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Januari 2016. Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Kapombe alicheza dakika zote 180 za mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo Shooting. Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania Prisons ilikuwa kiporo, na ilichezwa Februari24, 2016. Kapombe alifunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 wa timu yake dhidi ya Mgambo Shooting. Pia alisaidia kupatikana bao la Azam kwenye mechi dhidi ya African Sports iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, na mara nyingi mashambulizi ya timu yake yalianzia upande wake. Washindani wa Kapombe kwenye kinyang’anyiro hicho katika mwezi huo walikuwa mshambuliaji wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Jeremiah Juma na beki wa Coastal Union ya Tanga, Miraji Adam. Kwa kutwaa tuzo hiyo, Kapombe atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni

Ligi Kuu Uingereza, Leicester yang’ang’ania kileleni

Leonardo Ulloa aliipatia ushindi Leicester dakika ya 89 ya mchezo dhidi ya Norwich City Ligi Kuu Uingereza imeendelea siku ya Jumamosi kwa kuwa na michezo sita ambapo vinara Leicester City iliendelea kujiimarisha kileleni baada ya kuifunga Norwich 1-0 katika dimba la King Power. Nao mabingwa watetezi Chelsea waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Southampton katika Uwanja wa St. Mary. Leonardo Ulloa alishindwa kuficha furaha yake baada ya kuipatia ushindi Leicester City Matokeo mengine ni kama ifuatavyo; Jumamosi 27 Februari 2016 West Ham 1 – 0 Sunderland Leicester 1 – 0 Norwich Southampton 1 – 2 Chelsea Stoke 2 – 1 Aston Villa Watford 0 – 0 Bournemouth West Brom 3 – 2 Crystal Palace Jumapili 28 Februari 2016 Liverpool v Everton 15:00 Newcastle v Man City 15:00 Man Utd v Arsenal 17:05 Tottenham v Swansea 17:05 Muda wote ni kwa saa za Afrika Mashariki

Walimu Dar kusafiri bure

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda Katika kumuunga mkono Rais Dk. John Magufuli kutekeleza mpango wa elimu bure, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria jijini Dar es Salaam,  wameamua walimu wa shule za msingi na sekondari kuanzia Machi 7, mwaka huu, kutolipa nauli katika daladala. Mpango huo utaanza kutumika baada ya kukamilika utengenezaji wa vitambulisho maalumu kwa waalimu hao wanaokadiriwa kuwa 10,000. “Ninawatangazia wananchi kuwa kuanzia Machi 7, mwaka huu, walimu wa sekondari na msingi watasafiri bure katika vyombo vya usafiri katika jiji letu la Dar es Salaam,” alisema Makonda. Mwenyekiti wa Chama cha Wasafirishaji Dar es Salaam (Darcoboa), Sabri Mabruki, alisema makubaliano hayo ni kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Magufuli katika kutekeleza mpango wa elimu bure na kupunguza makali ya maisha kwa walimu hao. Alisema walimu wataanza kusafiri bure kuanzia saa 11:30 alfajiri hadi saa mbili asubuh

Kutoka Face Boook leo mchana

Elizabeth Gilbert‎  FAIDA 10 ZA MAYAI KIAFYA (1) Mayai yana virutubisho vya kushangaza. (2) Mayai huwa na kolesto nyingi lakini hayaathiri kolesto katika damu. (3) Mayai huuongeza Msongamano wa juu wa lipoprotini kolesteroli (Kolesto nzuri). (4) Mayai yana kiinilishe mhimu sana kiitwacho ‘Choline’. (5) Mayai hubadili   msongamano wa chini wa lipoprotini kolesto. (6) Mayai huondoa sumu na kusaidia kuongeza nuru ya macho (7) Mayai yenye kiasi kingi cha Omega-3 husaidia kupunguza mafuta yapatikanayo katika damu (triglycerides). (8) Mayai yana protini yenye ubora wa hali ya juu na amino asidi mhimu kwa uwiano mzuri. (9) Mayai hayaleti ugonjwa wa moyo na yanaweza kupunguza hatari ya kupatwa na Stroke. (10) Mayai humtosheleza mlaji kwa haraka na hivyo kusaidia kupunguza uzito

Platnumz ashinda tuzo mbili nchini Uganda

Msanii Diamond Platnumz anazidi kukusanya tuzo barani Afrika, usiku wa kuamkia January 31 ameshinda tuzo mbili katika tuzo za Hipipo AWARD za nchini Uganda. Diamond ameshinda tuzo ya Nyimbo bora ya Afrika ya Mashariki na video bora ya Afrika ya Mashariki. Katika Mtandao wa Instagram, Diamond Platnumz ameandika “Awards tonight on @HipipoAwardsUGANDA…EAST AFRICA SUPER HIT#NANA and EAST AFRICA BEST VIDEO#NANA many thanks to my brother@2niteflavour @i_am_godfather and all Behind this Hit!!!… thanks alot @HIPIPOAwards for keep supporting the real African talent! (Wadau kijana wenu nimefanikiwa kushinda tunzo mbili Usiku wa leo kama NYIMBO BORA AFRICA MASHARIKI#NANA na VIDEO BORA AFRICA MASHARIKI #NANA nawashkuru sana kwa kura na support zote mnazoendelea kunipa….. tafadhali nisaidieni kuhesabu ni tunzo ngapi tumechkua tangu Mwaka 2016 uanze? ) shukran sana@tommyleeafrica kwa kuiwakilisha vyema @Wcb_wasafi Ugan

Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) umetoa bilioni 24 kushughulikia wakimbizi kutoka Burundi

Tanzania yapewa bilioni 24 kwa lengo la kushughulikia mahitaji ya wakimbizi kutoka Burundi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametoa dola za Marekani milioni 100 (US$ 100m, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 220) kutoka katika Mfuko Mkuu wa Kushughulikia Dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF) kwa shughuli za misaada katika maeneo tisa yenye dharura duniani na yasiyo na fedha za kutosha.  Tanzania ambayo kihistoria imepokea mamilioni ya wakimbizi kutoka nchi jirani kwa miaka mingi imetengewa dola za Marekani milioni 11 (Sawa na shilingi za Tanzania bilioni 24) kutoka katika kiasi hicho kwa lengo la kushughulikia mahitaji ya wakimbizi kutoka Burundi. Zaidi ya raia 126,000 wa Burundi wamekimbilia nchini Tanzania tangu mwezi Aprili, 2015, kufuatia machafuko ya kisiasa nchini humo. Huku tayari wakimbizi 64,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) wakiwa tayari nchini na kufanya jumla idadi ya  wakimbizi 193,000 nchini. Kutokan

record ya peke yakeeeee Super coach Jackson Mayanja

mtibwa 1-0 jkt ruvu 2-0 Burkinafaso 3-0 African sports 4-0