Beki Shomari Kapombe wa timu ya Azam FC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Januari 2016.
Katika mwezi huo uliokuwa na raundi tatu, Kapombe alicheza dakika
zote 180 za mechi mbili za timu yake dhidi ya African Sports na Mgambo
Shooting. Mechi ya tatu ya Azam FC katika raundi hiyo dhidi ya Tanzania
Prisons ilikuwa kiporo, na ilichezwa Februari24, 2016.
Kapombe alifunga mabao yote mawili kwenye ushindi wa mabao 2-1 wa
timu yake dhidi ya Mgambo Shooting. Pia alisaidia kupatikana bao la Azam
kwenye mechi dhidi ya African Sports iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1,
na mara nyingi mashambulizi ya timu yake yalianzia upande wake.
Washindani wa Kapombe kwenye kinyang’anyiro hicho katika mwezi huo
walikuwa mshambuliaji wa Tanzania Prisons ya Mbeya, Jeremiah Juma na
beki wa Coastal Union ya Tanga, Miraji Adam.
Kwa kutwaa tuzo hiyo, Kapombe atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000
(milioni moja) na wadhamini wa Ligi hiyo Kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom Tanzania Limited.
Comments