Skip to main content

Posts

Showing posts from July, 2011

HOTUBA YA MHE. GODBLESS JONATHAN LEMA (MB)

MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WIZARA YA MAMBO YA NDANI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012. Mheshimiwa Godbless Lema Mbunge Jimbo la Arusha Mjini -Chadema --- UTANGULIZI -- Mheshimiwa Spika, kwa maslahi ya umma wa Watanzania, napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwepo hapa leo, kuwasilisha Maoni na Mapendekezo ya Kambi rasmi ya Upinzani, kuhusu Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa mujibu wa kanuni ya 99(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2007. Mheshimiwa Spika, natoa pia shukurani zangu za dhati kwa familia yangu, Mke wangu Neema Lema, watoto wangu, Allbless Lema na Brilliant Lema, na wazazi wangu wote, Mzee Elibariki Jonathan Lema na Mama . Mheshimiwa Spika, napenda pia kutoa shukrani zangu za dhati kwa wapiga kura wangu wa Jimbo la Arusha Mjini kwa imani yao kwangu. Licha ya vitisho, vipigo na mabomu ya machozi yaliyotawala kampeni na hata siku ya kupiga, kuhesabu ku

Lovers’ Island

Produced by Javed Jafferji - Directed by Bond Bin Sulieman ZG Films , led by renowned photographer and filmmaker Javed Jafferji, aims to not only meet and surpass the current standard of filmmaking in Tanzania, but to raise the bar to such an extent that it re-invents the Tanzanian movie scene and ushers in a new era of worldclass film production in the country. As evidence of achieving this goal, ZG Films presented a rare double billing at this year’s Zanzibar International Film Festival. With Journey to the State House: The Life of Seif Shariff Hamad and Glamour: The Reality Behind Dreams , ZG Films is presenting itself as the leader in Tanzanian film production. Now ZG Films is preparing to release it’s second feature film of 2011: Lovers’ Island tells the story of a couple who have lost the spark in their marriage. In an effort to get it back and save their marriage they decide to find a tropical island, a island perfect for lovers in their position, where th

Ramadhan: Ratiba Ya Futari Washington

| RATIBA YA FUTARI YA PAMOJA WASHINTON DC www.tamcousa.org Assalam Alaykum, Ndugu waislamu Uongozi wa Tanzanian Muslim Community in Washngton DC Metro(TAMCO) unawakaribisha na kuwajulisha kuwa kama kwaida yetu kwa mwezi wa Ramadhani tutakuwa tukifuturu pamoja jumammosi na jumapili zote za Mwezi wa Ramadhani. Tunaombwa tuudhurie na tuwajulishe wengine wote: SAT. 08/06/11 – Sligo Avenue Neighborhood Park Adress: 500 Sligo Avenue, Silver Spring, MD 20910 XXXXXXXX SUN.08/07/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park SAT.08/13/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park SUN.08/14/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park SAT.08/20/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park SUN.08/21/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park SAT.08/27/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park SUN.08/28/11 – Hillandale PAB - Hillandale Local Park Address: Hillandale PAB - Hillandale Local Park: 10615 New Hampshire Avenue, Silver Spring, MD 20903 XXXXXXX TAMCO EID DAY: SAT. 09/05/11 – H

Tanzania Na Afrika Kusini Zatiliana Saini Mkataba Wa Ushirikiano Kiutamaduni

Waziri wa Habari,Utamaduni na michezo Dr.Emmanuel Nchimbi na Mwenyeji wake Waziri wa Utamaduni wa Afrika ya Kusini Paul Mashatile wakisaini mkataba wa kuanzishwa rasmi ushirikiano katika Nyanja ya utamaduni kati ya Afrika ya kusini na Tanzania jana jijini Pretoria huku Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Afrika ya kusini Jackob Zuma wakishuhudia ... Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua katika viwanja vya kumbukumbu ya mshujaa waliopigania uhuru wa Afrika ya Kusini nje kidogo ya jiji la Pretoria jana. Wapili kushoto ni Mama Salma Kikwete na watatu kulia ni mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini.Rais Kikwete yupo nchini Afrika ya Kusini kwa Ziara rasmi ya Kitaifa ya Siku mbili... Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Jackob Zuma wa Afrika ya Kusini wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Zuma kwa heshima yake wakati wa kilele cha Ziara Rasmi ya siku mbili nchini humo(Picha Zote; Freddy Maro )

Rostam Aziz Ajivua Gamba Rasmi jana-Aachia Nafasi zake Zote Hadi Ubunge

Aliyekua Mbunge wa Igunga-CCM Rostam Aziz -- HOTUBA YA MHE.ROSTAM AZIZ KWA WAZEE WA IGUNGA TABORA LEO UTANGULIZI WAZEE wangu, kwanza kabisa kabla ya kueleza kile ambacho kimenisukuma kuzungumza nanyi leo,napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu,mwingi wa rehema kwa kutuwezesha kufikia siku hii ambayo inatukutanisha waja wake. Wazee wangu wa Igunga,baada ya kufanya hivyo napenda pia kutumia fursa hii kuwashukuru ninyi nyote mmoja mmoja na katika umoja wenu kwa kuitikia wito wangu,kijana wenu, niliyewaomba nije nizungumze nanyi siku hii ya leo. Nafanya hivyo nikitambua vyema kwamba,kama si nyinyi wazee wangu na wengine wengi ambao hatuko nao hapa leo kwa sababu mbalimbali, ambao mmekuwa na imani kubwa nami nisingeweza kufikia hapa nilipofika sasa. Wazee wangu, waasisi wa taifa letu walitufundisha kutambua na kuheshimu ukweli kwamba; ‘Uongozi ni Dhamana’dhana ambayo kila ninapokaa na kutafakari huwa inanirejesha nyuma na kukumbuka jinsi nyinyi mlivyokaa katika umoja wenu