pichani katikati ni Batarokota akiwa na Watu Wa Gola
Kundi la muziki wa kizazi kipya linaloitw Mambo Club Talent On la mjini Morogoro linalo kuja kwa kasi nchini Tanzania, siku ya tarehe 13/07/2011 limekamilisha kurekodi video ya wimbo wao mpya `Tusherekee Pamoja` ambao umerekodiwa chini mtayarishaji mahiri aitwaye Kassanda .
Nyimbo hiyo `Tusherekee Pamoja iliyo rekodiwa audio katika studio ya Tush Record ya jijini Morogoro nakufanikiwa kutoka ndani ya mwezi wa sita mwaka huu ambapo imeanza kushika chati katika vituo mbalimbali ndani na nje ya nchi. akiongea na blogu hii msanii mmoja wa kundi hilo, Batarokota alisema picha za matukio y ya video hiyo zimechukuliwa katika Hotel ya Motel Biaf na Mambo Club zote za mjini humo kwa msaada wa wadhamini Mambo Club, Motel Biaf, na Batarokota Entertainment.
Comments