Skip to main content

Posts

Showing posts from June, 2011

BASATA :Ngoma Za Asili Zipo, Zina Hadhi Na Nafasi Kubwa

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema kwamba,ngoma za asili bado zina hadhi na nafasi kubwa katika jamii zetu ingawa kwa maeneo ya mijini mwamko wa sanaa hiyo unaonekana kupungua tofauti na zamani. Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao makuu ya Baraza hilo Ilala Sharif Shamba,Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba,ngoma za asili zipo kama kawaida na zimekuwa na nafasi kubwa mikoani ambako zimekuwa zikivuta watu wengi. “Kuna matamasha makubwa ya ngoma za asili kama yale ya Makuya, ya kale yanapokutana na ya sasa, Bujora na Chamwino.Matamasha haya yamekuwa yakivuta watu wengi sana hivyo,dhana kwamba ngoma za asili zimetoweka si sahihi” alisema Materego. Aliongeza kwamba,kinachotokea kwa sasa ni athari za utandawazi kwenye ngoma za asili ambazo zimebadili upepo wa sanaa hiyo maeneo ya mijini lakini akasisitiza kwamba,bado hata maeneo ya mijini kuna vikundi vingi vya ngoma za asili vinavyofanya vizuri. “Utandawa

Kutoka Baraza La Wawakilishi:Bajeti Ya Wizara Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar Yapitishwa

MWAKILISHI wa Magomeni Salimin Awadh akitaka maelezo ya matumizi ya komoja ya Vifungu vya bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wakati wa kupitisha vifungu vya Wizara hiyo jana. MWAKILISHI wa Mji Mkongwe Ismail Jussa akitaka ufafanuzi wa kimoja cha kifungu cha Wazari hiyo wakati wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais. Hija Hassan Hija( KIWANI) akitaka ufafanuzi wa kifungu cha bajeti wakati wa kupitisha bajeti ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Mamamu wa Kwanza wa Rais .Picha na Othman Maulid-Zanzibar

NAPE ANACHANJA MBUNGA !

MAMIA ya wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mtwara 28/6.2011.... Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, CCM, Nape Nnauye akijadiliana jambo na Mbunge wa Lindi mjini, Hasnain Mohammed Murj wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Mtwara 28/6/2011... Aliyekuwa mwanachama wa CUF na mgombea udiwani kwa tiketi ya chama hicho katika uchaguzi mkuu uliopita, Mohamed Chiungulumana akikabidhi kadi ya chama hicho kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipotangaza kurejea CCM kwenye mkutano uliofanyika 28/6/2011 mjini Mtwara. Jumla ya wanachama 154 wa CUF walijiunga na CCM katika mkutano huo.Kuhsoto ni Katibu wa NEC Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma. Picha zote: Bashir Nkoromo

TAARIFA YA MAZISHI YA EDGER KILEKE ( KAKA DICK) LEICESTER UK

Ndugu, Jamaa, na Marafiki, Watanzania wote: Tunapenda kuwa taarifu kwamba mazishi ya ndugu yetu marehemu Edgar Kileke (Kaka Dick) yatafanyika: JUMATANO Tarehe 29 June 2011 IBADA ITAFANYIKA: LEICESTER CENTRAL SEVENTH DAY ADVENTIST CHURCH LONDON ROAD LE2 1EF LEICESTER MUDA: SAA NNE KAMILI ASUBUHI (10AM) MAZIISH YATAFNYIKA: GILROES CEMETRY Na baada ya mazishi kutakuwa na huduma ndogo kwa wafiwa yaku toa shukurani: 85 STEVENSON DRIVE LE3 9AD Kwa Maelezo zaidi wasiliana na: NDUGU Assa Ali 07951644936 au Fauzia Musa 07943962628 Asanteni sana na Mungu awabariki. R.I.P EDGAR -- Be Cheerful! GOD loves you more than you'll ever know

Vodacom Miss Pwani Yafana

Vodacom Miss Pwani Winifrida Gracian katikati akiwa na mshindi wa pili Thuraiya Dabas(kushoto) na mshindi watatu Mariaclara Mathayo kwenye shindano hilo lililofanyika jana katika ukumbi wa TASUBA,Pwani Wilaya ya Bagamoyo. Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude kulia akimkabidhi zawadi ya shilingi 100,000 mshindi wa tatu Mariaclara Mathayo,shindano hilo lililofanyika jana katika ukumbi wa TASUBA,Pwani Wilaya ya Bagamoyo. Afisa tawala Wilaya ya Bagamoyo Daniel Machunda akimkabidhi zawadi ya shilingi 250,000 mshindi wa Vodacom Miss Pwani Winifrida Gracian mara baada ya kunyakua taji la shindano hilo lililofanyika jana katika ukumbi wa TASUBA,Pwani Wilaya ya Bagamoyo. Warembo tano bora waliotinga katika kinyanganyiro cha Vodacom Miss Pwani,shindano hilo lilifanyika hapo jana katika ukumbi wa TASUBA,Pwani Wilaya ya Bagamoyo. Mtaalam wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu kushoto,Afisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim K

JK Akutana Na Mkurugenzi Wa Peace Corps

1.Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Bwana Aaron Williams, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la huduma za kujitolea za Wamarekani (American Peace Corps)ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi wakati mkurugenzi huyo na ujumbe walipomtembelea na baadaye kufanya mazungumzo. 2. Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt, wakiweka saini katika ramani ya duania inayoonyesha sehemu mbali mbali duniani ambapo Shirika la huduma za kujitolea za Wamarekani(American Peace Corps volunteer) linatoa huduma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu shirika hili lilipoanzishwa.Wengine katika picha aliyesimama kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo duniani, Bwana Aaron Wiliams, na kulia,a liyesimama ni Mkurugenzi wa shikika hilo nchini Bi.Andrea Wojnar Diagne. Shirika la Peace Corps lilianzishwa mnamo Tarehe moja Machi mwaka 1961 na aliyekuwa Rais wa Marekani hayati John F.Kennedy. Hapa nchini jumla ya wanacham

TASWA YALAANI MASHABIKI WA MOTEMA PEMBE KUMDHALILISHA MWANDISHI WA JAMBO LEO.

CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimesikitishwa na kinalaani tukio lililomkumba mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la JamboLeo, Asha Kigundula wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba na DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jumapili iliyopita. Mwandishi huyo pamoja na Watanzania wengine waliokuwa Kinshasa, DRC kushuhudia mchezo wa Simba na DC Motema Pembe kwenye Uwanja wa Mashujaa ‘Stade des Martyrs’ walifanyiwa fujo ambazo hatukutarajia kama mashabiki wenye busara wangeweza kuzifanya. Kilichotusikitisha zaidi ni hatua ya mashabiki hao kumdhalilisha mwandishi huyo bila kujali utu wake, heshima yake na thamani yake, kisa tu ni Mtanzania ambaye alikuwa uwanjani hapo kushuhudia timu ya Tanzania ikicheza. Kamati ya Utendaji ya TASWA itakutana haraka iwezekanavyo kuhusiana na tukio hili ili kupata maelezo ya kina kwa vile Katibu Mkuu wa chama, Amir Mhando alikuwepo Kinshasa

OFISI YA BUNGE YATOA TAARIFA JUU YA HABARI ILIYOCHAPISHWA NA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA…

YAH: TAARIFA POTOFU YA GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA TOLEO LA JUMATATU, 20 – 26 JUNI, 2011 ‘ SAKATA LA POSHO ZA WABUNGE’ SPIKA MAKINDA MBUMBUMBU ‘Utafiti wabaini anasimamia asichokijua magwiji wa Bunge washangaa tamko lake’. 1.0UTANGULIZI Pamoja na Vichwa vya habari hiyo, Katika taarifa hiyo Mwandishi wa gazeti hilo amedai kuwa; i.Spika wa Bunge, Anne Makinda hana uelewa wa kutosha wa jinsi mbunge anavyoweza kupoteza wadhifa wake ii.Pia Spika wa Bunge haelewi mfumo wa malipo ya Posho za Wabunge iii.Spika hana mamlaka ya kumfukuza Mbunge yeyote anayekataa kusaini Fomu za kuchukua posho ya kikao. 2.0MAJIBU YA HOJA POTOFU ZILIZOTOLEWA Ofisi ya Bunge ingependa kuwaarifu wananchi kwamba habari hiyo iliyoandikwa na gazeti la Dira ya Mtanzania ni ya dharau na haina ukweli wowote na imeandikwa kwa nia mbaya ya uchochezi na kuharibu sifa aliyonayo Mhe. Spika Bungeni na kwa watanzania kwa ujumla. Ili kuondoa upotofu wa taarifa iliyotolewa na gazeti hili, Ofisi ya Bun

HELLO !

Dogo Rama (kushoto) akiwa na Janet wote kutoka African Stars aka Twanga Pepeta wakizungumza kwa njia ya simu , hapa ni Club Bilicanas (nyuma ya stage)

Rais Kikwete Ziarani Seychelles

| R ais Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Seychelles Mheshimiwa James Manchan kwenye uwanja wa mpira wa mjini Victoria,mji mkuu wa Seychelles wakati wa kuadhimisha sherehe za siku ya Taifa hilo tarehe 18.6.2011. Rais Jakaya Kikwete akipokewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Seychelles Mheshimiwa James Alix Michel mara tu baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Victoria nchini humo tarehe 18.6.2011 kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Rais Jakaya Kikwete akipokewa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Seychelles Mheshimiwa James Alix Michel mara tu baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Victoria nchini humo tarehe 18.6.2011 kwa ziara ya kikazi ya siku moja. Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Seychelles Mheshimiwa James Michel kweye ikulu ya nchi hiyo mjini Victoria tarehe 18.6.2011 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mke wa Rais wa Seychelles Mama Natalie Mic

Former president Chiluba is dead

Second President of Zambia Fredrick Titus Jacob Chiluba has died. Chiluba died of a heart attack in the early hours of today, Saturday, shortly after mid night. His pokeperson Emmanuel Mwamba confirmed that Chiluba died at his home in Kabulonga, in the capital Lusaka. He explained that Chiluba was with his lawyers most of the time on Friday but only fell ill in the evenning. Doctors checked on him but said it was nothing serious. But at midnight he got serious and died. Frederick Jacob Titus Chiluba born April 30, 1943 was the second President of Zambia from 1991 to 2002. Chiluba, a trade union leader, won the country’s multi-party presidential election in 1991 as the candidate of the Movement for Multiparty Democracy (MMD), defeating long-time President Kenneth Kaunda . He was re-elected in 1996. His former Vice President Levy Mwanawasa , also late, succeeded him. After leaving office, Chiluba was the subject of a long investigation and trial regarding alleged corrupti

PRESIDENT JAKAYA KIKWETE IN GENEVA…!!!

The International Labour Organisation (ILO) Director General Juan Somavia welcomes to the ILO Headquarters President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete . President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete addresses the 100 th session of the ILO in Geneva, Switzerland yesterday.Photos By Freddy Maro-State House

KATIBU MKUU WA CCM, WILSON MUKAMA AKUTANA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA MSUYA, NAKUMTEBELEA MUFTI WA TANZANIA SHEIKH MKUU ISSA BIN SHAABAN SIMBA

Picha juu Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama(Kulia)akimkaribisha ofisini kwake, Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya,leo Mtaa wa Lumumba mjini Dar es Salaam... Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa Bin Shaaban Simba, akimkaribisha Ofisini kwake, Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama, jana,Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Tanzania Uingereza Peter Kallaghe Audhuria ''TROPPING THE COLOUR EVENT'

Balozi Peter kallaghe akiwa na familia yake nje ofisi na makazi ya waziri mkuu Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallaghe pamoja na familia yake wakati walipoudhuria Parade Maalum inayofanytika kila mwaka kuadhimisha siku ya kuzaliwa Malkia wa Uingereza Queen Elizabeth II Parade ya Nguvu walikia wa Uingereza Queen Elizabeth IIakiwa katika gari maalum linalovutwa na farasi kuingia viwanjani hapo

MHE.OMAR YUSSUF MZEE ATOA MUELEKEO WA BAJETI YA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi, Mipango na Maendeleo Zanzibar Omar Yussuf Mzee akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar, kuhusiana na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2011 - 2012. WAANDISHI wa Habari wa Vyombo mbalimbali wakimsikiliza Waziri Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi Mipango na Maendeleo Zanzibar wakivuatilia maelezo ya Waziri kuhusu muelekeo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2011 - 2012 ,Wizara ya Fedha Vuga. NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Abdi Khamis Faki, Mhasibu Mkuu wa Serikali Zanzibar Omar Hassan (King) wakimsikilizaWaziri akitowa Muelekeo wa Bajeti.Picha na Othman Maulid-Zanzibar

MKUTANO WA WADAU WA KUJADILI BAJETI

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini, Peter Mziray akichangia maoni mjadala wa Bajeti ya Serikali ya 20011/2012 iliyoandaliwa na Kituo cha Demokrasia (TCD), Dar es Salaam Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC-CCM), Ramadhan Madabida akichangia maoni wakati wa mjadala wa Bajeti ya Serikali ya 20011/2012 iliyoandaliwa na Kituo cha Demokrasia (TCD), Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia akiongoza mjadala wa Bajeti ya Serikali ya 20011/2012 iliyoandiliyoandaliwa na Kituo hicho, Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kituo hicho, Profesa Ibrahim Lipumba akifungua mkutano huo wa mjadala wa bajet.Picha zote na Mdau Richard Mwaikenda

Christina William Ndie Vodacom Miss Iringa 2011

Christina William Ametwaa Taji La Vodacom Miss Iringa 2011 Katika Kinyang’anyiro Cha Ulimbwende Kilichofanyika Kwenye Ukumbi Wa Highland Manispaa ya Iringa huku Ritha Justine Nafasi Ya Pili Na Zay Mselemu Nafasi Ya Tatu, Happiness James Nafasi Ya Nne Na Ya Tano Ni Jackline Erick. Picha: Misanjo Livigha

Makamu Wa Rais Dkt. Gharib Bilal Katika Mkutano Wa UN

| Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya viongozi wenzake kutoka nchi mbalimbali wakati akishiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi unaofanyikajijini New York jana. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mahojiano na mtangazaji wa Redio ya Umoja wa Mataifa (UN), Flora Nducha, muda mfupi baada ya kuhudhuria mkutano wa majadiliano kuhusu masuala ya ukimwi ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa unaofanyika jijini New York, Juni 10, 2011, jijini New York. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Tacaids, Dkt. Fatma Mrisho (kushoto) na Mkurugenzi wa Tume ya Ukimwi Zanzibar, Dkt. Omari Shauri (kulia) wakati walipomtembelea Makamu wa rais jijini New York Juni 9 na kufanya mazungumzo. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

Makamu Wa Rais Tanzania Akutana Na Ban ki Moon

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Ban Ki Moon, wakati alipokutana naye kwa mazungumzo ofisini kwake jijini New York, jana Juni 8, 2011 baada ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi, unaoendelea. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha Rose Migiro, akisalimiana na Naibu waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakati waziri huyo alipoongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katika ofisi ya Umoja wa Mataifa (UN) New York kwa ajili ya mazungumzo . Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi, unaoendelea jijini New York Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.