Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2012

ZANZIBAR YAIKALISHA RWANDA NAMBOOLE

Khamis Mcha ‘Vialli’ akiruka kushangilia baada ya kufunga bao la kwanza. Kushoto ni Jaku Juma. Na Mahmoud Zubeiry, Kampala MABAO mawili ya kiungo wa Azam FC, Khamis Mcha ‘Vialli’ usiku huu yameipa Zanzibar ushindi wa 2-1 dhidi ya Rwanda, katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala. Kwa ushindi huo, Zanzibar Heroes imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya michuano hii, ikipanda kileleni mwa Kundi hilo, kwa pointi zake nne, Rwanda ikishuka nafasi ya pili kwa pointi zake tatu, sawa na Malawi, wakati Eritrea inashika mkia kwa pointi yake moja. Vialli alifunga mabao yake moja kila kipindi, la kwanza dakika ya sita na la pili dakika ya 61, yote akionyesha yeye ni fundi na mwenye akili na maarifa ya soka kutokana na kutulia na kumtungua kipa hodari kabisa katika ukanda huu, Jean Claude Ndoli. Rwanda ilipata ba

WAZIRI WA HABARI AFUNGUA MKUTANO WA MA-RAS JIJINI DAR LEO

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifungua Mkutano baina ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wajumbe wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania Bara “Ma-RAS” (hawapo pichani) Jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unalengo la kujadili maendeleo ya Michezo nchini. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akisalimiana na RAS wa Njombe mara baada ya kufungua kufungua Mkutano baina ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na wajumbe wa Kamati za Michezo za Mikoa Tanzania Bara Ma-RAS Jijini Dar es Salaam.Mkutano huo unalengo la kujadili maendeleo ya Michezo nchini. (Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM).

Jaji Chande Aikwepa Kesi Ya Lema

 JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Othman Chande amejitoa kusikiliza rufaa ya kesi ya aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, badala yake nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda. Kujitoa kwa jaji mkuu kumekuja ikiwa zimebaki siku tano kusikilizwa upya kwa rufaa hiyo Desemba 4, mwaka huu, baada ya awali Mahakama ya Rufani, kuona rufaa hiyo ilikuwa na dosari. Mahakama hiyo ilikubali hoja ya wajiburufaa kuwa rufaa hiyo ilikuwa na dosari kutokana na tofauti ya vifungu vya sheria vilivyotumika katika hukumu iliyomvua ubunge Lema na vilivyotumika katika hati ya kukaza hukumu, iliyowasilishwa mahakamani sambamba na rufaa hiyo. Hata hivyo, kilichomwokoa Lema ni kifungu cha 111 cha Kanuni za Mahakama, ambapo mahakama hiyo ilisema kuwa chini ya kanuni hiyo, dosari hizo zinaweza kurekebishwa. Jaji Chande ndiye aliyekuwa ki

Mwamvita Makamba Na Watoto Yatima...!

                               Picha na A ljabry Bukhite

MILLARD AYO AKIFANYA MAHOJIANO NA MZEE MAJUTO MSIBANI MUHEZASASA HIVI...!

Jamaa yuko huko na blogu hii inaendelea kufuatilia kwa karibu.Asante Millard  kwa picha.

Washukiwa wa ICC Kenya kuunda Muungano

Uhuru Kenyatta ni mmoja wa washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007   Washukiwa wawili wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya, Uhuru Kenyatta na William Ruto wanajadiliana kwa lengo la kuunda muungano wa kisiasa watakaotumia kugombea uongozi wa nchi. Taarifa za awali zilisema kuwa wawili hao tayari wameunda muungano huo ingawa baadaye afisa wa mawasiliano wa vigogo hao alikana kuwepo makubaliano yoyote. Wawili hao ambao ni mahasimu wa jadi kisiasa,wanaanda mkutano wa pamoja siku ya Jumamosi mjini Nakuru mojawapo ya maeneo yaliyokumbwa na ghasia mbaya zaidi za kikabila baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007. Na hataua ya wawili hawa inakuja wakati mahakama ikitarajiwa kutoa uamuzi kuhusu ikiwa wanaweza kugombea uongozi wakati wanakbiliwa na tuhuma za kuhusikana ghasia za baada ya uchaguzi ambapo mamia ya watu waliuawa. Wanasema wameamua kuunda muungano watakaoutumia kuwania nafasi ya rais na makamu wake katika uchaguzi mkuu mwaka u

Wakazi wasaidia kusafisha mabaki ya al-Shabaab Mogadishu

By Majid Ahmed, Mogadishu Wakazi wa Mogadishu wanafanya jukumu kubwa katika usafishaji wa mabaki ya al-Shabaab katika mji mkuu, maofisa wa usalama wa Somalia wamesema. Washukiwa wa Al-Shabaab wakipanda katika gari ndogo ya wazi ya polisi tarehe 10 Oktoba, mwaka 2012 katika kituo cha polisi huko Mogadishu ya kusini. [Abdurashid Abdulle Abikar/AFP] Fununu kutoka kwa wakazi katika eneo la Yaqshid huko Mogadishu ya kaskazini Jumamosi (tarehe 24 Novemba) ilisababisha katika kukamatwa kwa washukiwa 21 wa al-Shabaab na ugunduzi wa maficho ya silaha, kwa mujibu wa maofisa usalama. Siku mbili kabla, vikosi vya usalama vilifanya operesheni kutokana na fununu kutoka kwa mmiliki wa shamba huko Yaqshid ambayo matokeo yake ilikuwa mauaji ya kamanda wa al-Shabaab Abdinur Gardhub . Operesheni ya tarehe 22 mwezi Novemba pia ilisababisha kukamatwa kwa wanamgambo wengine 16 ambao walifanya shughuli nje ya kikundi kidogo cha watu katika maeneo ya Yaqshid, Suqa Holaha

Arafat’s grave opened, experts seek evidence of poison

Arafat, who led the Palestinians’ bid for a state through years of war and peacemaking, died in Paris aged 75 in 2004 after a short, mysterious illness. (Reuters) By JIHAN ABDALLA, REUTERS RAMALLAH The body of the late Palestinian leader Yasser Arafat was exhumed on Tuesday by a team of international experts trying to discover if he was poisoned, as many Palestinians believe. French magistrates opened a murder inquiry in August into Arafat’s death in Paris after a Swiss institute said it had discovered high levels of radioactive polonium on his clothing, which was supplied by his widow, Suha. Arafat, who led the Palestinians’ bid for a state through years of war and peacemaking, died in Paris aged 75 in 2004 after a short, mysterious illness. No autopsy was carried out at the time, at the request of Suha, and French doctors who treated him said they were unable to determine the cause of death. But allegations of foul play immediately surface

Magazeti Leo Jumatano

  Kwa hisani ya Mjengwa.

SHILINGI BILIONI 86 ZAIBWA WIZARA YA NISHATI/TANESCO, GRIDI YA TAIFA HATARINI

Na Zitto Kabwe Gazeti la The East African la Novemba 24 – 30, 2012 limetoa taarifa kwamba jumla ya dola za kimarekani milioni 54 zimegundulika kuibwa na watumishi waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la TANESCO kupitia manunuzi ya Mafuta ya kuendesha mtambo wa Umeme wa IPTL. Gazeti hili limenukuu taarifa ya ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Tanzania (Controller and Auditor General). Taarifa hiyo inasema kuna kikundi (racket) ambacho kazi yake kubwa ni kujifaidisha binafsi na mpango wa umeme wa dharura kupitia manunuzi ya Mafuta mazito ya IPTL. Itakumbukwa kwamba toka mwaka 2011 kumekuwa na shinikizo lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba zabuni za ununuzi wa mafuta ya kuendesha mpango wa umeme wa dharura na mchakato mzima wa manunuzi ya mafuta haya ufanyiwe uchunguzi wa kina (forensic audit). Katika mkutano wa 3 wa Bun

PICHA YA GOLDIE NA NAVIO WAKITENGENEZA VIDEO - AFRIKA KUSINI.

. .

NIYONZIMA AING'ARISHA RWANDA KAMPALA

Nahodha wa Rwanda, Haruna Niyonzima (katikati) akidhibitiwa na wachezaji wa Malawi, katika mchezo wa Kundi C, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge 2012 uliofanyika kwenye Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda usiku huu. Rwanda ilishinda 2-0, mabao ya Jean Baptiste Mugiraneza dakika ya 37 na Haruna Niyonzima dakika ya 79. Wachezaji wa Rwanda wakishangilia bao lao la kwanza ushindi. Source Bin Zubeiry Blogspot.com.

STUDENT’S SPECIAL BASH YATIKISHA DAR LIVE KWA WASANII WA NGUVU

Fid Q na Stamina wakifanya makamuzi ya hatari jukwaani. Dullayo akiwapelekesha puta mashabiki. Rich Mavoko akionyesha cheche zake jukwaani. Kala Jeremiah akiwapagawisha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live. Stamina akiwatuliza mzuka mashabiki. P Square wa Bongo (waliovaa ‘jeans’ na miwani) na madansa wao, wakilishambulia jukwaa. Tano Bora wa shindano la The Mic King wakiwa katika picha ya pamoja.

CHALENJI… BOCCO ATUPIA MBILI

  Mshambuliaji wa timu ya Kilimajaro Stars, Simon Msuva akimfungisha tela beki wa timu ya taifa ya Sudan, Faris Abdallah wakati wa mechi yao ya Kundi B la michuano ya Kombe la Chalenji kwenye Uwanja wa Namboole mjini Kampala jana jioni.Kwa hisani ya www.fullshangweblog.com

Shetta akiwa ndani Club Maisha Jana Usiku

Kinyerezi Maeneo ya hali ya Hewa Kwa Mdau Ikiwa ni Sehemu za Bata za Wikiend Jana

 Hapa ilikuwa ni sehemu ya stori zenye bashasha na huku bata zikiendelea kwa kwenda mbele. k l Anaitwa Francis Mrema  ndiye mdau anaye miliki The Blue Point iliyoko  maeneo ya hali ya hewa  akiwa mzigoni  . Hapa wadau wakipiga stori za hapa na pale  huku bata za 'kufamtu ' zikiendelea . Ilikuwa ni wikiendi iliyofanyika kwa kiwango cha juu kabisa pembezoni mwa mji wa Dar maeneo ya Kinyelezi hali ya Hewa.

Na Gazeti la Mwananchi: Ridhiwan, Lowassa waelezea utajiri wao

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwan wamezungumzia tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwao kwamba wanamiliki rasilimali zenye thamani ya mabilioni ya shilingi. Ridhiwan Kikwete Lowassa kwa upande wake amekuwa akidaiwa kuwa tajiri anayemiliki kampuni kubwa za kibiashara na kumekuwa na taarifa kwamba ana ukwasi ambao vyanzo vyake vinatia shaka na siyo rahisi kuvitolea maelezo. Kwa upande wake Ridhiwan naye amekuwa akidaiwa kuwa na utajiri mkubwa na amekuwa akihusishwa na biashara za kampuni za kusafirisha mafuta ambayo hupelekwa kwenye migodi, umiliki wa hoteli na majengo kadhaa ya kifahari. Wote wawili wamekuwa wakidaiwa kwamba baadhi ya mali zao wamekuwa wakiziendesha chini ya kivuli cha wafanyabiashara wengine wakubwa nchini ili kukwepa kuhojiwa walikotoa utajiri huo, taarifa ambazo hata hivyo imekuwa vigumu kuzithibitisha. Hata hivyo jana kwa nyakati na mazingira tofauti, Lowassa na Ridhiwan walijitok

Balozi Seif avalia njuga masuala ya umiliki wa ardhi, Serikali yafuta hati ya umiliki

Na Othman Khamis Ame, OMPR Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kumfutia mara moja hati ya umiliki wa Eneo la Shamba la Serikali Bwana Abeid Said Shankar alilopewa katika Kijiji cha Sehemu kufuatia mgongano unaoendelea kujitokeza kati yake na Wana kijiji wa eneo hilo ambao unaashiria hatma mbaya ya kuvunjika kwa amani baina ya pande hizo mbili. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Ndugu Juma Ali Juma na Ofisa wake wa Kilimo wakimuonyesha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif eneo la Ramani ya Shamba la Wizara hiyo la ekari 6 linaloleta mzozo wa umiliki. Serikali pia imeuzuia Uongozi wa Kituo cha Kujiendeleza Kielimu cha Eneo hilo kufanya shuguli yoyote ya ujenzi kwa vile umiliki wake hauko kihalali katika vyombo vinavyosimamia masuala ya Ardhi. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara fupi katika eneo hilo ambapo alishuhudia mgongano na malalamiko ya Wananchi hao dhidi ya wawa

Somali forces kill top al-Shabaab commander

The Somalia National Army (SNA), backed by its intelligence and the Police force, have conducted a raid on Sokohola and killed the overall al-Shabaab commander for Gupta, Sokohola, and Huluwai areas. Somali National Army The al-Shabaab fighters put up a fight, but their commander, who residents identified as Guludupu, was killed on spot, while 16 militants were captured and an assortment of ammunition recovered in the Thursday night raid. They included 16 submachine guns and four pistols. Sokohola, a Mogadishu suburb, has been a concentration area of al-Shabaab cells, terrorising civilians around Mogadishu, the Somalia capital city. The African Union Mission in Somalia (AMISOM) — Uganda contingent commander, Brig. Michael Ondoga commended the Somali security forces for “excellence in their operations.” “The Somali national security forces are doing a commendable job in the pacification process of Somalia. As AMISOM, we are committed in giving th

The blue point inakuletea siku ya Nyama choma-25.11.2012

 The blue point na wadau mbali mbali inakualika ....Ile siku inawadia na punde imekaribia yenye shuguli nzito na ya kipekee yaani nyamachoma huku tukiangalia Dunia kupitia Dstv ni jumapili ya Tarehe 25.11.2012 kuanzia saa 12:00 mchana  njoo wewe mwenziao na wote ... mtajihudumia wenyewe .. local  beer 2.00 @ 8,000 kwa 1' kg , karibu  sana  endelea kutembelea kila mara www.machibya.blogspot.com ili kukujuza habari hizi. Hapa ni Full Bataa.     Managing Director/Marketing Manager. Francis A.Mrema akiwa kazini. Office: Fran`s Traders. P.o Box 63094. Dar Es Salaam, TANZANIA. Tel/Fax: +255 783 22 55 78 Kinyerezi Mwisho-Kifuru to Hali ya hewa.   Nyama Choma , si pakukosa kesho mdau.   Personal Contact: Francis A.Mrema. P.o Box 63094, Dar Es Salaam. TANZANIA. +255 (o) 713 225578 +255 (o) 767 225578 Email:faam76@yahoo.com