Viongozi wa Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa sauti
moja wamelitaka kundi la waasi la M23 lililouteka mji wa Goma siku ya
Jumatatu usiku, kuondoka nmjini humo na hawatokubali mapinduzi dhidi ya
serikali yeyote ya kanda ya maziwa makuu.
Rais Museveni wa Uganda akiuliza watafanya nini ikiwa kundi litakata kuondoka alisema "wataona chamtema kuni".
Marais Yoweri Museveni, Paul Kagame na Joseph Kabila walizungumza na
waandishi habari baada ya mazungumzo yao na kueleza kwamba ingawa
wapiganaji wa M23 wanamadai yaliyo ya haki lakini hawawezi kutumia nguvu
kupindua serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.
Rais Kabila amesema yuko tayari kuyasikiliza malalamiko ya waasi na atafanya kila awezalo kuyashughulikia.
Kwa Upande wake rais Kagame amesema kuhudhuria kwake mazungumzo hayo
kunamaanisha anataka amani kwa kanda nzima, bila ya kutilia maanani sula
la waandishi habari ikiwa anawaunga mkono wapiganaji wa M23.
Source: voaswahili.com
Comments