Ndege
za Israel zimeshambulia majengo ya serikali ya chama cha Hamas huko
Gaza ikiwemo ofisi ya waziri mkuu baada ya baraza la mawaziri la Israel
kuidhinisha kuitwa kwa wanajeshi wa akiba 75,000 kuvamia Gaza.
Ndege hizo za Israel zimeshambulia wizara ya ulinzi na jengo la ofisi ya
Waziri Mkuu Ismail Haniyeh ambapo hapo Ijumaa alikutana na Waziri Mkuu
wa Misri. Kwa siku kadhaa miripuko mizito imekuwa ikilitingisha eneo la
Gaza linalokaliwa na idadi kubwa ya watu na kusababisha kufuka kwa moshi
mzito angani.
Hamas yaendelea kurusha maroketi
Wanamgambo wa itikadi kali za Kiislamu nao wamekuwa wakiendelea
kuvurumiosha maroketi nchini Israel. Licha ya machafuko hayo,waziri wa
mambo ya nje wa Tunisia amewasili Gaza leo hii kuonyesha
mshikamanona na Wapalestina na kushutumu mashambulizi hayo ya Israel kuwa sio halali na yasiokubalika.
Maafisa huko Gaza wanasema Wapalestina 41 wakiwemo raia 20 watoto wanane
na mwanamke mmoja mjamzito wameuwawa katika huko Gaza tokea Israel
ilipoanza operesheni zake siku nne zilizopita.Raia watatu wa Israel
wameuwawa na shambulio la roketi hapo Alhamisi.
Jeshi la Israel limesema kikosi chake cha anga kimeshambulia takriban
maeneo 180 waliokuwa wameyalenga jana usiku ikiwa ni pamoja na makao
makuu ya polisi majengo ya serikali,vikosi vya kurusha maroketi na kituo
cha mafunzo cha Hamas katika Ukanda huo wa Gaza uliozongwa na umaskini.
Jengo la ghorofa tatu la afisa wa Hamas Abu Hassan Salah pia
lilishambuliwa na kuharibiwa kabisa mapema leo alfajiri. Waokoaji
wamesema takriban watu 30 wametolewa kwenye kifusi cha jengo hilo.
Comments