Tanzania ina idadi kubwa ya watu ambao hawana
njia ya moja kwa moja ya kupata umeme, wakati asilimia 50 ya watanzania
wanamiliki simu za mkononi. Ili kuchaji simu zao inawalazimu kwenda kwa watu wao
wa karibu kama vile ndugu, jamaa, marafiki au wakati mwingine kwenye vibanda na
madukani.
Ofisa Masoko wa kampuni ya
Tigo Jacqeuline Nnunduma (kushoto) na Meneja Mradi wa Kampuni hiyo, Yaya
N'dojere pamoja na Ofisa Uhusiano Msaidizi wa Tigo, Mariamu Mlangwa wakionesha
kifaa cha solar kinavyoweza kufanya kazi ya kuchajishia simu kwa njia ya nishati
ya jua.
Kwa vile asilimia kubwa ya watu hawa ni wateja
wa Tigo, tumeamua kuyapa maduka yetu vifaaa vya nishati ya jua vyenye uwezo wa
kuchaji simu. Kwa njia hii mteja wa Tigo kamwe hatakuwa na tatizo la simu yake
kuishiwa chaji kwa ajili ya kukosa umeme.
Kwa wateja wa Tigo ambao wanaishi mbali na
vyanzo vya umeme, huduma hii bunifu inarahisisha na kufanya upatikanaji wa
bidhaa za Tigo uwe rahisi, pamoja na kuwapa wateja nishati rafiki na endelevu,
kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku .
Kwa kupitia vifaa vya nishati ya jua ambavyo
vitakuwa vikipatikana katika maduka ya Tigo, Tigo inaendelea kuwajali wateja
wake ambao wanaendesha maisha na hata biashara zao katika maeneo yasiyo na
umeme. Wateja watalipia kiasi nafuu cha shilingi 300 kila watakapohitaji kuchaji
simu zao.
Kwa wamiliki wa maduka hayo ya Tigo, Tigo
inatoa huduma za teknolojia mpya katika soko la Tanzania ili kuwasaidia
wajasiriamali kupanua biashara zao na halikadhalika inaongeza kipato chao.
Wanaohitaji kujisajili kwa ajili ya vifaa
wanaweza kutuma barua pepe solar@tigo.co.tz. Kigezo kinachohitajika ni
kutokuwepo kwa umeme kwenye eneo husika au muhusika awe anauza chaji za
simu.
Comments