Mahakama
ya Wilaya ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar leo imepunguza masharti ya
dhamana kwa Viongozi saba wa Jumuiya mbili za Kiislamu Zanzibar,
wanaokabiliwa na mashtaka ya kusababisha vurugu na kupelekea uharibifu
wa miundombinu ya barabara mjini Zanzibar, leo tena wameshindwa kupata
dhamana.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina,
amesema kuwa uwamuzi huo umetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mh. Ame
Pinja, baada ya kukubali maombi ya Mawakili wa Watuhumiwa waliomba
kupunguzwa kwa masharti hayo kwa wateja wao.
Watuhumiwa
hao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimam ZanzibarSheike Farid Hadi Ahamed
na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe Mselem Ali Mselemu na wenzao
watano.
Inspekta
Mhina amesema kuwa kutokana na uwamuzi huo, kila mshitakiwa sasa
atatakiwa kuwa na wadhaminiwa wawili ambao ni watumishi wa Serikali na
kwa kila mmoja awe na kiasi cha shilingi 500,000 tofauti na mashrti ya
awali ya wadhamini watatu na kwa kila mmoja kwa kiasi cha shilingi
milioni moja kwa kila mmoja.
Hata
hivyo pamoja na kupunguzwa kwa masharti hayo, hakuna hata mshitakiwa
mmoja aliyedhaminiwa kutokana na kukosekana kwa wadhamini ambao ni
watumishi wa serikali.
Inspekta
Mhina amesema kuwa Watuhumiwa hao ambao wanakabiliwa na kesi tatu
tofauti za kuzusha ghasia na kupelekea vurugu katika maeneo mbalimbali
ya mji wa Zanzibar, wamerudishwa rumande hadi desemba 4, mwaka huu kesi
yao itakapotajwa tena.
Amesema
wakati wote mahakama hiyo ikiiendelea, hali ya ulinzi nje na ndani ya
Mahamakama uliimarishwa vya kutosha ambapo Makachero wa Jeshi la Polisi
pamoja na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia na wale wa vikosi.vya
Ulinzi vya Zanzibar.Chanzo:fullshangweblog
Comments