Na: Habari Maelezo Zanzibar 07/11/2012
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ametiliana saini makubalianao ya mwanzo (Memorandum of Understanding )na Jumuiya ya Kimataifa ya Kuhifadhi Haki Miliki(world intellectual property organization –wipo)) juu ya kuanzisha nembo yake kwa zao la karafuu na mengine.
Kwa upande wa Zanzibar ulitiwa sainai na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Ahmed Nassor Mazrui na kwa upande wa WIPO ulitiwa saini na mwakilishi wake Neema Nyerere na mwakilishi wa Kituo cha Kimataifa cha Biashara ( ITC) Jacky Charbonneau.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Waziri wa Biashara amesema kuwa Zanzibar itafaidika sana katika mpango huo kwani utaweza kulinda zao lake la karafuu na pia kuitangaza Zazibar katika Ulimwengu.
Amesema kuwa na Nembo ya kibiashara kutaweka hadhi ya mazao yetu katika soko la Dunia na nchi nyengine na pia kukinga nchi nyengine kutumia mazo yetu kwa njia zisizo halali.
Aliwahakikishia uwajibikaji wa serikali ya mapinduzi Zanzibar juu ya suala hilo ili kuona kwamba linafanikiwa na kwamba yale malengo yaliliyowekwa ya kiutaalam, kiufundi na kisayansi yanafanikiwa.
Kuingia katika jumuiya hiyo hatua kadhaa zinahitajika kuchukuliwa katika zao zima la karafuu kuanzia ukulima wake, ukaushaji, uhifadhi mapaka usafirishaji wake ili kuona kwamba kiwango chake hakipungui na kuleta athari katika masoko.
Hivyo alisema ni muhimu kwa wakulima wataalam wa kilimo wa zao la karafuu na mazao mengine kupata taaluma ya kutosha katika uzalishaji wa mazao hasa hayo ya viungo. Amesisitiza kwamba wakati umefika wa kufanya mapinduzi ya zao la karafuu na kuachana na njia zisizo sahihi za uwanikaji na utunzaji wa zao hilo.
Mapema mwakilishi wa WIPO Neema Nyerere alizitaka Bodi za Viwango Zanzibar kuwa makini katika kupasisha Bidhaa kwani bila ya bidhaa kuwa na viwango vinavyotakiwa kimataifa hakutaweza kulinda soko na kudumisha sifa ya bidhaa yenyewe na nchi pia. Hivyo alizitaka Taasisi hizo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi ili malengo yaliowekwa yaweze kufikiwa.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 07/11/2012
Comments