Uhaba wa mafuta ya petroli na dizeli ambao umeendelea kuukumba mji
wa Iringa kwa zaidi ya siku tano sasa, umeendelea kuwatesa wananchi
wa kada mbalimbali ambapo jana, Mbunge wa jimbo la Wawi katika
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed (CUF) ameonja
keor hiyo baada ya kuingia mjini Iringa na kujikuta akisota kwa zaidi
ya saa nne katika foleni ya kusubiri kununua mafuta katika kituo cha
kimoja wapo kilichokuwa kikiuza mafuta katika eneo la Ipogolo.
Hamad Rashid (katikati) akitazama picha katika iPad yake alizopiga foleni hiyo ya mafuta mjini Iringa leo
Mbunge Hamad alikuwa safarini kutokea mkoani Morogoro akielekea Mafinga wilaya ya Mufindi ameieleza francisgodwin blog
kuwa serikali inapaswa kuangalia uwezekano wa kutatua tatizo hilo
la uhaba wa mafuta hapa nchini vinginevyo uchumi wa nchi utaendelea
kuyumba zaidi.
Francis Godwin (kofia nyekundu) akihojiana na Mhe. Hamad huko Iringa jana.
Amesema kuwa kitendo cha wananchi kushinda katika foleni kwa saa
zaidi ya sita wakisubiri kununua mafuta katika kituo hicho ni sawa na
wananchi hao kupoteza muda wa kuzalisha, hivyo Serikali iliyopo
madarakani inapaswa kushughulikia tatizo hilo ambalo linasababishwa na
waagizaji wakubwa wa mafuta hapa nchini.
Mbunge huyo alisema alifika katika foleni hiyo majira ya saa 8 mchana na kufanikiwa kununua mafuta saa 12 jioni.
Mbali ya uhaba huo wa mafuta, uchunguzi uliofanywa na Francis Godwin
umebaini kuwa baadhi ya vijana walikuwa wakishirikiana na
wafanyakazi wa vituo hivyo vya mafuta kwa kununua mafuta na kujaza
katika mapipa na kupakia katika magari na kwenda kuyauza kwa bei kubwa
zaidi mjini Iringa.
Foleni ya mafuta leo huku baadhi wakifanya hujuma kwa kununua kwa bei ya kawaida na kwenda kuuza kwa bei kubwa
Chanzo wavuti.com
Comments