By Majid Ahmed, Mogadishu
Wakazi wa Mogadishu wanafanya jukumu kubwa katika usafishaji wa mabaki
ya al-Shabaab katika mji mkuu, maofisa wa usalama wa Somalia wamesema.
Washukiwa wa Al-Shabaab wakipanda katika
gari ndogo ya wazi ya polisi tarehe 10 Oktoba, mwaka 2012 katika kituo
cha polisi huko Mogadishu ya kusini. [Abdurashid Abdulle Abikar/AFP]
Fununu kutoka kwa wakazi katika eneo la Yaqshid huko Mogadishu ya
kaskazini Jumamosi (tarehe 24 Novemba) ilisababisha katika kukamatwa kwa
washukiwa 21 wa al-Shabaab na ugunduzi wa maficho ya silaha, kwa mujibu
wa maofisa usalama.
Siku mbili kabla, vikosi vya usalama vilifanya operesheni kutokana na
fununu kutoka kwa mmiliki wa shamba huko Yaqshid ambayo matokeo yake
ilikuwa mauaji ya kamanda wa al-Shabaab Abdinur Gardhub . Operesheni ya
tarehe 22 mwezi Novemba pia ilisababisha kukamatwa kwa wanamgambo
wengine 16 ambao walifanya shughuli nje ya kikundi kidogo cha watu
katika maeneo ya Yaqshid, Suqa Holaha na Gubta, kwa mujibu wa kamanda wa
Idara ya Usalama wa Taifa huko Benadir Koloneli Khalif Ahmed Ereg.
Ereg alisema maficho ya al-Shabaab huko Yaqshid yaligundulika kutokana na taarifa zilizotolewa na wakazi wa eneo hilo.
"Vikosi vya usalama viliwatia kizuizini wanachama 37 wa kikundi cha
wapinga amani wa al- Shabaab, wakati wa mfululizo wa mashambulizi ya
usiku yaliyofanywa kitongoji cha kaskazini ya Mogadishu," Ereg aliiambia
Sabahi. "Mashambulizi haya yalilenga katika usafishaji wa mabaki ya
al-Shabaab katika eneo hilo."
"Operesheni hizi zilisababisha kunyang'anywa kwa maficho ya aina tofauti
za silaha ikiwa ni pamoja na silaha za vita, bunduki AK-47, silaha,
milipuko na maguruneti ya kurusha kwa mkono," alisema.
Comments