Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Joyce Mapunjo
akizungumza na wahitimu 2882 wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam
(CBE) wakati wa mahafali ya 47 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika
viwanja vya Mnazi mmoja jana jioni Jijini Dar es salaam na kuwataka
kutumia elimu yao kujiajiri na kuwa chachu ya maendeleo nchini.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam (CBE) Bw. Athman Ahmed (kulia)
akitoa taarifa kuhusu mahafali ya 47 na maendeleo ya chuo hicho kwa
mgeni rasmi wa mahafali hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara Bi. Joyce Mapunjo (katikati).
Wahitimu wa mahafali ya 47 ya Chuo cha CBE wakifuatilia masuala
mbalimbali yaliyokua yakiendelea wakati wa mahafali hayo katika viwanja
vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Picha
no 5. Baadhi ya wananchi na wapiga picha wa kujitegemea waliohudhuria
mahafali ya 47 ya Chuo cha CBE sehemu ya Dar es salaam wakiendelea
kufuatilia matukio mbalimbali wakati wa sherehe hizo.
Picha na habari na Aron Msigwa – MAELEZO.
Comments