Juhudi za mwanzo za kupatikana makubaliano juu ya bajeti ya mwaka 2013 ya umoja wa Ulaya zimeshindwa.
Serikali za mataifa ya umoja huo pamoja na bunge zimeshindwa kupata
msimamo wa pamoja kuhusu suala la utendaji baada ya karibu saa nane za
mazungumzo jana Ijumaa(09.11.2012).
Pande hizo mbili zitajaribu tena kupata makubaliano siku ya Jumanne,
kabla ya muda wa mwisho ambao ni usiku wa manane , kuweza kukubaliana
juu ya bajeti ama kuirejesha halmashauri ya Ulaya , katika kazi ya
kuipanga upya bajeti hiyo.
Wanasiasa wa umoja wa Ulaya hawatilii manani sana uchelewesho huo, na wana matumaini kuwa muda wa mwisho unaweza kufikiwa.
Jumanne ndio mwisho
"Ni pale tu ambapo hatutaweza kufanikiwa siku ya Jumanne, tuwe watulivu
na hatupaswi kujiuliza kuhusu nia njema ya wadau wote," amesema Adreas
Mavroyiannis, naibu waziri anayehusika na masuala ya ulaya kutoka
Cyprus, nchi ambayo kwa sasa inashikilia urais wa kupokezana wa umoja wa
Ulaya.
"Inatokea katika wakati wa muafaka kuwa kuna kuwa na hali ya mkwamo ,
wasi wasi," amesema kamishna wa bajeti ya umoja wa ulaya Janusz
Lewandowski. "lakini nafikiri hali ya uwajibikaji ipo."
Mavroyiannis, hata hivyo , amesema kuwa hali ya kuweza kushindwa siku ya Jumanne "haiwezi kuondolewa kabisa".
Comments