Skip to main content

Posts

Showing posts from November, 2018

Mo Dewiji aipongeza Simba kwa kuibuka na ushindi Taifa

Mfanya biashara maarufu nchini Mohamed Dewij ambaye pia ni muwekezaji katika timu ya Simba amefunguka mengi baada ya ushindi wa Simba juzi dhidi ya Mbabane kutoka nchini Swatziland ambaye kwa sasa inaitwa Eswatini. Mo Dewij ambaye ndio mara yake ya kwanza kwenda uwanjani kuangalia mpira na baada ya mchezo aliandika maneno haya:-  ” Hongereni Simba kwa ushindi! Kwa kweli wachezaji wetu wamejituma. Sasa tujipange kwa mchezo wa marudiano wiki ijayo. Lengo letu ni kuwa Mabingwa wa Afrika! Isha’Allah tutafanikiwa siku moja hivi karibuni.  #ThisIsSIMBA   #NguvuMoja  “

BENKI YA KCB TANZANIA YANDAA SEMINA ‘BIASHARA CLUB’ KWA WAFANYA BIASHARA WADOGO NA WAKATI (SME)

KCB Bank Tanzania jana iliendesha  kongamano la Biashara Club kwa mara ya pili mwaka 2018 jijini Mwanza, Tanzania. Hii ni baada ya kuendesha kongamano kama hili lililofana kwa wafanyabiashara zaidi ya 200 jijini Dar es Salaam mapema mwaka huu.  Pichani ni Ms. Lightness Mlay, KCB Bank Trade Sales Manager answers questions from Mwanza business owners and executives  during the KCB Bank Biashara Club Workshop held at Gold Crest Hotel in Mwanza on 29th November 2018. The event attended by more than 150 businesses in the SME sector aimed to build capacity on matters of finance management, record keeping and tax compliance.  Bi. Lightness May, Meneja wa Mauzo ya Kibiashara wa Benki ya KCB akijibu maswali kutoka kwa wafanyabiashara wa jiji la Mwanza katika hafla ya Biashara Club Workshop iliyofanyika Gold Crest Hotel tarehe 29.11.2018 jijini Mwanza. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 200 ilikuwa na lengo la kutoa mafunzo katika maswala ya usimamizi wa fedh

Sikia ya jayo ya Diamond

Msanii wa muziki Diamond Platnumz yupo kwenye mazungumzo na mmoja kati ya wadau wa muziki kutoka Afrika Kusini kwaajili ya kutengeneza ukumbi wa burudani Dar es salaam. Akizungumza na chanzo kimoja ambacho si blog hii , mmoja kati Wakurugenzi wa Wasafi Festival, Mkubwa Fella amesema tayari Diamond ameshazungumza na mdau huyo kutoka Afrika Kusini na yupo tayari kutumia zaidi ya tsh bilioni 1 kwaajili ya ujenzi wa ukumbi huo mkubwa. “Baada ya kukutana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa tumemkumbusha tena kwamba kama tutapata uwanja, tunaweza kujenga ukumbi wa burudani, tumepata mwekezaji ambaye yupo tayari kuwekeza zaidi ya tsh bilioni 1,”

Rais Dkt. John Pombe Magufuli jinsi alivyo fungua Maktaba Mpya kubwa na ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli juzi tarehe 27 Novemba, 2018 amefungua maktaba mpya, kubwa na ya kisasa ya Chuo  Kikuu cha Dar es Salaam iliyojengwa katika Kampasi Mlimani (Mwl. Julius K. Nyerere) Jijini Dar es Salaam. Maktaba hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati imejengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 93.6 ikiwa ni msaada kutoka Serikali ya China na inakuwa maktaba kubwa kuliko maktaba zote ambazo China imezijenga barani Afrika. Katika taarifa yake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye amesema majengo ya maktaba hiyo yenye ghorofa mbili yamechukua eneo lenye ukubwa wa meta za mraba 20,000 yakiwa na uwezo wa kuhifadhi vitabu 800,000, kukalisha watumiaji 2,100 kwa wakati mmoja, yana kompyuta 160 zilizounganishwa na mtandao kwa ajili ya kusoma vitabu kwa njia ya kielektroniki, ofisi za wafanyakazi, eneo la wanafunzi wenye mahitaji maalum na ukumbi wa kisasa wa mihadhara wenye uwezo wa kuchukua watu 600.

Azam FC mawindoni dhidi ya Stand United

  Azam FC maarufu kama wana lambalamba wameanza rasmi mazoezi  tayari kuanza safari ya kuzisaka pointi kuelekea mchezo ujao dhidi ya Stand United. Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utafanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Desemba 4 mwaka huu, ambapo Azam FC iko kwenye mwenendo mzuri baada ya kushinda mechi saba mfululizo za ligi hiyo. Wachezaji wote wa Azam FC wameripoti mazoezini wakiwa na hali nzuri kabisa isipokuwa kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’, ambaye ni mgonjwa. Beki wa kulia Nickolas Wadada, aliyekuwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda, naye amesharejea kundini akiwa ni miongoni mwa wachezaji walioripoti kwenye mazoezi hayo. Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuendelea na mazoezi kwa wiki hii yote, na siku ya Jumamosi wanatajia  kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya vijana ya timu hiyo (Azam U-20) kwa ajili ya kujiweka sawa utakaopigwa asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex.. Azam FC inayonolewa na Kocha Mholanzi Hans Van D

Vodacom Tanzania Foundation imekuwa mstari wa mbele kuchangia vifaatiba katika vituo vya afya nahospitali hapa nchini ilikuokoa maisha ya watoto njiti.

  Pichani ni  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom Plc Tanzania Bi Jacquiline Materu akikabidhi mashine na vifaa vya hospitali ya kambi ya Nyarugusu kwa Katibu tawala wa Wilaya ya Kasulu, Titus Luguha katika kambi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki iliyopita. Vifaa hivyo vyenye thamani ya TZS milioni 25 vimetolewa na Taasisi ya Vodacom Foundation kwa hospitali hiyo ili kuongeza juhudi za kuhakikisha watoto wanaozaliwa njiti katika kambi hiyo wanaishi. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi ya Doris Mollel, Bi Doris Mollel na wa nne kushoto ni Mkuu wa kambi hiyo Bw. Francis Chokola. Pichani ni  Katibu tawala wa Wilaya ya Kasulu, Titus Luguha, akimfunika moja kati ya wakimbizi waliojifungua watoto njiti katika kambi ya Nyarugusu misaada iliyotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa kambi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita. Nyuma yake ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi Jacquiline Materu, M

Leo magazetini

Atletico Madrid na Barcelona kikaangoni

Klabu za Atletico Madrid na Barcelona huenda zikapigwa faini ya Euro €3,000 hadi €6,000 kwa makosa ya utovu wa nidhamu, yaliyojitokeza kwenye mchezo wao wa Ligi uliopigwa wikiendi iliyopita. Kamati ya ushindani ya La Liga imesema kwenye mchezo huo uliomalizika kwa klabu hizo kutoka sare ya  1-1 . Barcelona walichelewa kuingia uwanjani kipindi cha pili, huku Atletico hao mashabiki wao walirusha chupa uwanjani. Mashabiki wa Atletico Madrid walianza kurusha chupa Uwanjani,  baada ya Dembele kufunga goli la kusawazisha dakika za mwisho za mchezo huo.

Waziri wa Kilimo nchini Josephat Hasunga awataka wakulima nchini kuongeza thamani ya mazao ya kilimo

WAZIRI wa Kilimo Josephat Hasunga amewataka wakulima nchini kuongeza thamani ya mazao    ya kilimo ili wakulima hao wanufaike zaidi. Ushauri huo ulitolewa na Waziri Hasunga jana alipo wahutubia wadau sekta binafsi ya kilimo nchini katika mkutano wa wadau hao uliofanyika Jijijini Dar es Salaam.   “Ni wakati wawakulima wetu kubadilika kwakuongeza thamani ya bidha ili kuhimili ushindani wa soko lakini hata kupata faida zaidi ,wakulima wetu wakifundishwa kusindika bidhaa zenye ubora kwakuzingatia usalama wa chakula tunaamini tutaleta mapinduzi ya sekta ya kilimo nchini,” amesema Hasunga. Hasunga alisema serikali kwakushirikiana na sekta binafsi wanayo mipango mingi ya kuboresha sekta ya kiliomo ambayo ndiyo sekta yenye mchango mkubwa kuliko sekta zote nchini. Aidha Hasunga amesema hali ya hakiba ya chakula nchini ni ya kuridhisha zaidi ambapo kwa mwaka huu kuna uzalishaji wa chakula kwa asilimia 125 na vikwazo mbalimbali ikiwemo utitiri ushuru ukiwa umeondolewa.

Wekundu wa msimbazi waipigia hesabu Mbabane Swallow FC ya Swaziland Ligi ya Mabingwa Afrika

Kuelekea katika mchezo wao wa jumatano dhidi ya Mbabane Swallow FC ya Swaziland wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba utakaochezwa uwanja wa taifa, Simba wameahidi makubwa kwa mashabiki. Kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye ni kipenzi cha mashabiki amesema maandalizi yapo vizuri kwa kuwa wamekuwa wakipewa mbinu mbalimbali ambazo zitawafanya waweze kupata matokeo katika mchezo huo. "Tupo vizuri wachezaji wote na tunatambua kuwa kazi iliyo mbele yetu ni kubwa, tunaomba Mungu tuweze kupata matokeo kwa kuwa hayo ndio malengo yetu kuweza kushinda mchezo wetu wa kimataifa. "Jumatano tutakuwa uwanjani, mashabiki wajitokeze kwa wingi maana wana umuhimu sana katika kufanikisha ushindi, watanzania kwa pamoja watupe sapoti katika mashindano haya ya kimataifa hatutawaagusha," alisema Mkude. Mbabane FC wanatarajiwa kutua leo kwa ajili ya mchezo huo wakiwa chini ya kocha wao wa muda kutoka Malawi ambaye aliwahi kuinoa Mbeya City, Kinah Phiri.

Rais Dk.Ali Mohamed Shein awasili Nairobi kuhudhuria Mkutano wa Blue Economy

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amewasili nchini Kenya kwa ajili ya kushiriki katika mkutano wa uchumi endelevu wa bahari(Sustaniable Blue Economy Confrence) utakaoanza kesho katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta Jijini Nairobi Nchini Kenya. Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Nairobi, Dk.Shein amepokelewa na viongozi mbali mbali wakuu wa Serikali ya Kenya wakiongozwa na balozi wa Kenya nchini Tanzania Dan Kanzungu pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dk. Pindi Chana. Katika ziara hiyo, Dk. Shein amefuatana na viongozi mbali mbali wa SMT na SMZ, akiwemo Waziri wa Kilimo Maliasili Mifungo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma,Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mhe.Dk.Sira Ubwa Mamboya,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Mazingira na Muungano Mhe January Makamba. Mkutano huo Mkubwa unaohusu sekta ya uchumi wa bahari ni wa kwanza kufanyika nchini Kenya, ambao u

Msuva aendelea kung'ara

KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva usiku wa jana ameifungia klabu yake, Difaa Hassan El- Jadidi katika sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji, Rapide Oued Zem kwenye mchezo wa wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro Uwanja wa Maniapaa ya Oued Zem. Msuva, mchezaji wa zamani wa Yanga SC aliye katika msimu wake wa pili Jadidi, alifunga bao lake dakika ya 31, kabla ya Issam Boudali kuisawazishia Rapide Oued Zem dakika ya 90 na ushei. Kwa matokeo hayo, Jadida inafikisha kwa pointi 10 baada ya kucheza mechi saba, ikiendelea kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi ya Morocco – na wapinzani wao, Rapide Oued Zem wanabaki nafasi ya sita kwa pointi zao 11 pia, ingawa wao wamecheza mechi nane sasa. Simon Msuva akikimbilia mpira jana Uwanja wa Maniapaa ya Oued Zem Simon Msuva (katikati) katika mchezo wa jana dhidi ya Rapide Oued Zem Simon Msuva katika kikosi cha Difaa Hassan El- Jadidi kilichoanza jana

Ukatili dhidi ya wanawake ni ugonjwa wa kimataifa unaoleta fedheha

Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni ugonjwa wa kimataifa unaoleta fedheha kubwa katika jamii zote duniani . Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake maalumu kuhusu siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ambayo huadhimishwa kila mwaka Novemba 25. Guterres amesema ugonjwa huo ni kinyume cha maadili kwa wanawake na wasichana wote, na ni kikwazo kikubwa  kwa maendeleo jumuishi , yaliyo sawa na endelevu. Katika msingi wake, ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni udhihirisho la ukosefu mkubwa wa heshima, kushindwa kwa wanaume kutambua usawa wa asili na utu wa wanawake. Ni suala la haki za msingi za binadamu. Amekumbusha kwamba ukatili unaweza kuchukua sura yoyote kuanzia ukatili majumbani, hadi usafirishaji haramu wa binadamu, kuanzia ukatili wa kingono katika miozo hadi ndoa za utotoni, ukeketaji na kuuawa. Ukatili huu unawaumiza watu binafsi na unaathari kubwa kwa familia na j

Mbagara Kuu n a viunga vyake wapo hatarini kuugua magonjwa ya mlipuko

WAKAZI wa Mbagara Kuu n   a viunga vyake wapo hatarini kuugua magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosekana kwa maji safi na salama takribani miezi tisa. Wakazi hao waliliambia gazeti hili kuwa adha hiyo ya upatikanaji wa maji imetokana na ujenzi wa Barabara zinazo boreshwa kwa kiwango cha lami katika mitaa ya Kata ya Mbagara kuu iliyo sababisha uharibifu wa miundo mbinu. Blog   hii ililifanya jitihada mahususi ili kupata maelezo ya kina kutoka kwa Kampuni zinazotekeleza ujenzi wa barabara hiyo ambazo ni Group six kutoka China na Harrising kutoka India lakini hawakupatikana. Kutokana na kutopatikana kwa wahusika wa Kampuni hizo mbili ambazo zinawajibika kurejesha miundo mbinu ya maji katika utaratibu wa kawaida na shughuli za ujenzi wa barabara ukiendelea Blog lilizungumza na Diwani wa kata hiyo Shaban Abubakari. Abubakari alikiri kuwepo kwa tatizo la upatikanaji wa maji katika mitaa ya Kata ya Mbagara Kuu ikiwemo Mbagara Kuu Magharibi, Kusini na Mgeni nani Kijichi ambapo baraba

Vodacom yazungumzia Uchumi wa Kidijitali

Pic 11: Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw Hisham Hendi akitoa mada kuhusiana na uchumi wa kidijitali kaatika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Pic 12: Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya Vodacom Tanzania, Bw Hisham Hendi akitoa mada kuhusiana na uchumi wa kidijitali katika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam. Nyuma ni Mkurugenzi wa Muendeshaji wa kampuni ya FSDT, Bi Irene Mlola na Mwenyekiti wa DTBi, Bw Mihayo Wilmore.  Pic 13: Mkurugenzi Mtendaji wa Universal Communication Service Access Fund (UCSAF), Peter Ulanga akizungumza katika mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Usimamizi wa Miradi (PMI) uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema jana. Mkutano huu umelenga kujadili ukuaji wa uchumi wa kidijitali.

Javier Aguirre amemtaka nyota wake Mo Salah kuwachana na klabu ya Liverpool

Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Javier Aguirre amemtaka nyota wake Mo Salah kuwachana na klabu ya Liverpool kama meneja wa klabu hiyo Jurgen Klopp atashindwa kutwaa taji msimu huu. Salah ambaye amefunga jumla ya mabao 44 msimu uliyopita amejikuta akiingia kwenye majeraha makubwa katika mchezo wa fainali ya Champions League walipokuwa wakiikabili Real Madrid. Kwa mujibu wa chombo cha habari cha The Sun, Aguirre amemtaka meneja Jurgen Klopp kuhakikisha anatwaa taji msimu huu kama anahitaji kuendelea kuwa na nyota huyo tegemezi wa Misri. Miamba ya soka ya Hispania Real Madrid imekuwa ikimtolea macho Salah kwa muda mrefu katika kunasa saini yake ili kuziba pengo la Cristiano Ronaldo. Licha ya kuwa Liverpool imetwaa mataji mawili tangu mwaka 2006, Aguirre amesema kuwa Salah yupo Anfield kwaajili ya kushinda mataji makubwa hivyo ni lazima kuangalia mbali zaidi kama yanashindikana. Hivyo ni vema kuachana na Liver kama ndani ya misimu huu itashindwa kutwaa mataji.

Mtibwa Suga michuano ya CAF Confederation Cup

Klabu ya Mtibwa Suga ya Turiani Morogoro inayowakilisha Tanzanaia katika michuano ya kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup) kwa msimu wa 2018/2019 wanatarajia kutumia Uwanja wa Azam Complex kama uwanja wao wa nyumbani. Michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi November 27 na 28 mwezi huu Mtibwa Sugar wamepangiwa kucheza dhidi ya Nothern Dynamos ya Usheli sheli. Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya kupeperusha bendera kimataifa katika mchezo wao wa kombe la Shirikisho dhidi ya timu ya Norhen Dynamo ya Shelisheli. "Tumebeba dhamana ya watanzania katika michuano hiyo kazi yetu kubwa ni kuweza kupata matokeo hilo ndilo jukumu ambalo nimewapa wachezaji wangu, wote wanalitambua hilo," alisema. Mtibwa Sugar wanaingia kwenye michuano hiyo baada ya kukamilisha adhabu yao ambayo walipewa ya kutoa faini baada ya kushindwa kupeleka timu kwenye michuano hiyo nchini Afrika kusini kutokana na Ukata