Wanasayansi nchini Uingereza na Gambia wanasema wana ushahidi wa awali unaoonesha kuwa mbwa wanaweza kunusa malaria. Wanasayansi hao wamewafunza mbwa kutambua harufu ya malaria kwa kutumia nguo za watu wenye maambukizi.
Kuna matumaini makubwa kuwa wanyama hao watatumika katika mapambano dhidi ya malaria na hatimaye kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.
Japokuwa
utafiti huo upo katika hatua za awali, wanasayansi wanaamini matokeo
yake yanaweza kubadili namna ya kufanya vipimo vya malaria.
Kwa
mujibu wa tafiti za hapo awali, mtu ambaye ana vimelea vya malaria
mwilini anakua na harufu ya tofauti ambayo inawavutia mbu kuendelea
kumshambulia. Na sasa, mbwa wapo kazini kuinusa harufu hiyo.
Soksi
zilizovaliwa na watoto usiku kucha katika jimbo moja nchini Gambia
zilisafirishwa mpaka Uingereza kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.
Kwa
mujibu wa BBC, Kati ya jozi 175 zilizotumwa katika wakfu wa mbwa wa
ugunduzi wa kimatibabu mjini Milton Keynes, 30 zilikuwa zimevaliwa na
watoto wenye vimelea vya malaria.
Mbwa hao wenye uwezo mkubwa wa
kunusa hivi sasa pia wapo kwenye mafunzo ya kunusa harufu ya saratani na
ugonjwa hatari wa kukakamaa (Parkinson’s disease).
Matokeo ya
jumla, ambayo yalitolewa katika mkutano wa mwaka wa Jumuiya ya Amerika
ya Magonjwa ya Kitropiki na Usafi yanaonesha kuwa kati ya watoto 10
walioathirika, mbwa wanauwezo wa kutambua watoto 7.
Lakini pia walifanya makosa kwa kudhani kuwa mtoto mmoja ana maambukizi kati ya 10 ambao wapo salama.
Mtafiti
Mkuu Profesa Steve Lindsay, kutoka chuo kikuu cha Durham, amesema
wanafuraha kubwa juu ya matokeo hayo, lakini mbwa hao bado hawajawa
tayari kutumika kila siku.
Watafiti bado wanahitaji muda zaidi
kuboresha umakini wa mbwa na kuanza kunusa watu badala ya soksi. Pia
wanata kujiridhisha kama mbwa wanaweza kutambua aina tofauti za malaria.
Comments