Vodacom Tanzania Foundation yakabidhi vifaa vya kulinda maisha ya watoto njiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma
14/11/2018, Dodoma, Tanzania- Katika kuunga mkono lengo
la serikali la kupunguza vifo vya uzazi na watoto njiti kwa kupunguza
uwiano wa vifo vya uzazi hadi kufikia watoto 292 kati ya watoto 100,000
kwa vizazi hai kutoka watoto 556 kati ya 100,000 ifikapo mwaka ....., Vodacom
Tanzania Foundation ikishirikiana na Doris Mollel Foundation imetoa mchango
wenye thamani ya TZS 25 milioni kwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma ili kulinda
maisha ya watoto njiti.
Pichani ni Waziri wa Madini Angellah Kairuki akiuliza swali kuhusu kitanda cha kuwaongezea joto Watoto njiti, kitanda hiki ni mojawapo kati ya vifaa tiba vyenye thamani Sh 25 m vilivyotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation vilivyokabidhiwa kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ili kusaidia kupunguza vifo vya Watoto Njiti. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia.
Tukio hili lilishuhudiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Waziri wa Madini
mheshimiwa Angellah Kairuki, na Mheshimiwa Antony Mavunde Naibu Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu.
Pichani ni Afisa Muuguzi Msaidizi kutoka Kitengo cha kuhudumia Watoto Njiti Constancia Mankupe akielezea kwa vitendo namna mashine ya kusaidia kupumua kwa Watoto njiti inavyofanya kazi, mashine hii ni mojawapo kati ya vifaa tiba vyenye thamani Sh 25 m vilivyotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation vilivyokabidhiwa kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ili kusaidia kupunguza vifo vya Watoto Njiti. Kulia kwake ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu Anthony Mavunde na Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel.
Msaadawetuunajumuisha vifaa muhimu vya kuokoa
maisha kama vile vifaa vya oksijeni (Oxygen concentrator) ambavyo vitasaidia
watoto njiti kupumua, thermometers 10, 4 weighing scales for infants, 40
branded bedsheets, baby warmer, 3 suction machines, ambu bag with facemasks for
infants, 1000 feeding tubes, phototheraphy machine, na vitanda vitatu vya
watoto. Mchango kama huo pia
utawasilishwa katika Kambi ya Wakimbizi iliyoko Nyarugusu Mkoani Kigoma.
Pichani ni Waziri wa Madini Angellah Kairuki (kulia) akizungumza wakati makabidhiano ya mashine ya kusaidia kupumua kwa Watoto njiti ilivyotolewa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ili kusaidia kupunguza vifo vya Watoto Njiti. Kushoto ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia, Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Doris Mollel (kati).
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Kitengo
cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom, Bi Rosalynn Mworia alisema,
"Vodacom imeazimia kupunguza idadi ya vifo vinavyotokea wakati wa
kujifungua pamoja na vifo vya watoto wachanga na inaunga mkono jitihada za
serikali za kuboresha utoaji wa huduma za afya. Tunatarajia kwamba mchango wetu
utaenda mbali katika safari nzima ya kuokoa maisha mengi zaidi ya wanawake na
watoto. "
Pichani ni Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation Rosalynn Mworia, akikabidhi mashine ya kusaidia kupumua kwa Watoto njiti kwa Waziri wa Madini Angellah Kairuki (wa pili kulia) na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayesimamia Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na walemavu Anthony Mavunde (kulia) katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma ili kusaidia kupunguza vifo vya Watoto Njiti. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel, Bi Doris Mollel.
Kwa upande wake, Mheshimiwa Ummy Mwalimu alisema,
"Mpango huu unakuja wakati muafaka ambapo serikali imeanza kampeni ya
kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na watoto wachanga
hapa nchini. Tunapenda kuwashukuru Vodacom Foundation na Doris Mollel
Foundation katika kusaidia nchi kukabiliana na changamoto hizi. Vifaa hivi
cheza nafasi muhimu katika kukabiliana na matatizo ambayo watoto njiti hukutana
nayo hasa katika wiki nne za kwanza za maisha yao."
Alitoa wito kwa wafanyakazi wa afya kuhakikisha matumizi
sahihi ya vifaa vya kuokoa maisha ya watoto njiti akisema, "Ninawasihi
wafanyakazi wa afya katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma kutumia kwa usahihi
vifaa hivi. Msiruhusu mashine zikusanye vumbi, mashine hizi ziko hapa kwa ajili
ya kuokoa maisha ya Watoto wetu. "
Pia alikuwepo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge
ambaye alisema kupambana na vifo vya watoto wachanga nchini Tanzania ni suala
mtambuka, maana ni wajibu wa kila mmoja wetu kwa pamoja. "Mchango huu ni
ishara kubwa ya ushirikiano kwa kampeni inayoendelea, Jiongeze - Tuwavushe
Salama na inalingana na kiapo nilichochukua, pamoja na Wakuu wengine wa Mikoa,
ambapo tuliahidi kufanya kazi ya kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga
nchini Tanzania kwa mujibu wa mkakati husika wa serikali chini ya Wizara
ya Afya. "Alisema.
Kwa upande wao, Mheshimiwa Angela Kairuki, na Mheshimiwa
Antony Mavunde, waliihimiza Vodacom Tanzania Foundation kuendelea na jitihada
za kusaidia wanawake na wasichana nchini kote kuboresha afya zao, kupata elimu
bora na kubuni miradi mipya.
Comments