Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma Giles Muroto, amethibitisha kutokea
vifo vya watu 7 katika ajali iliyohusisha magari mawili ya serikali
ikiwemo, STL 6250 Toyota Land Cruiser kutoka ofisi ya CAG, baada ya
kugongana uso kwa uso na gari yenye nambari SU 41173.
Kwa
mujibu kwa kamanda Muroto katika ajali hiyo ambayo imetokea usiku wa
kuamkia leo, pia watu watatu wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo na wamelazwa
katika hospitali za jirani zilizopo kwenye mkoa huo Dodoma kwa ajili ya
huduma ya kwanza na miili ya marehemu kwa ajili ya kuhifadhiwa.
“Hii
ajali inahusisha magari mawili ikiwemo Toyota Land Cruiser mali ya
ofisi ya CAG iliyokuwa na jumla ya watu 7 yaligongana uso kwa uso na SU
41173, Toyota Land Cruiser mnali ya NSSF ambayo ilikuwa na watu 3, na
kupelekea vifo vya watu 7 ajali ilitokea usiku wa kuamkia leo na jeshi
la polisi linaendelea kuchunguza kufahamu chanzo kiundani ”, amesema
Kamanda Mroto.
“Wito wangu kwa madereva ni hatari sana kusafiri
usiku, lakini pia tumepoteza vijana wa serikali na wamesomeshwa na
serikali, wito wetu magari yasafiri muda unaohitajika badala ya kusafiri
usiku, na tutaanza kuwa wakali zaidi sababu wengine wanasafiri usiku,
ili kukwepa tochi zetu”, amesema Kamanda Muroto
Comments