Skip to main content

Mambo 10 muhimu yaliyofanywa na Serikali ya awamu tano




Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli, imefanya jitihada kadhaa sambamba na kutekeleza  sera mbalimbali ambazo zimeiwezesha nchi ya Tanzania kupata mafaniko makubwa ndani na nje ya nchi katika kipindi  cha miaka mitatu.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, akizungumza leo jijini Dar es salaam , ametaja mambo 10 muhimu  yaliyofanywa na  Rais  Magufuli katika kipindi cha miaka mitatu na ambayo yameitangaza nchi ya Tanzania kimataifa.
Dkt. Abbasi alitaja mambo hayo kuwa ni uchumi unaoendelea kukua kwa kasi nzuri, ambapo  katika mwaka 2017/18 uchumi wa Tanzania ulikua kwa wastani wa asilimia 7.1 na kuongoza katika nchi zote za Afrika Mashariki, huku  ukiingia katika rekodi ya kuwa miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi duniani kama ambavyo  ripoti mbalimbali za kimataifa zimeeleza.
“Uchumi wetu ni wa tisa kwa ukuaji wa kasi duniani na katika Afrika, Kusini mwa Sahara ni wanne, hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya World Economic Forum ya mwezi  Machi, 2018 na kwa nchi za Afrika Mashariki  uchumi wa Tanzania unaongoza kwa ukuaji,” alisema Dkt. Abbasi.
Kuongezeka kwa mapato ya Serikali katika kipindi cha miaka mitatu, Rais Magufuli amethubutu kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuongeza kasi ya kukusanya kodi na hivyo kuongeza mapato ya kodi ya Serikali kutoka wastani wa shilingi  bilioni 850 kwa mwezi hadi kufikia wastani wa  shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi.
Kufufuliwa kwa mashirika ya umma, Dkt. Abbasi alisema kuwa kutokana na ufuatiliaji, ubunifu, uwekezaji wa Serikali ya Rais Magufuli, mashirika mengi  mfano  Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL), Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Mamkala ya Maji Safi (DAWASA) na Bandari  sasa yameanza kuamka kuwa na ufanisi, kuongeza mapato na mengine kutengeneza faida.
“Baadaa ya Serikali kuchagiza mageuzi ya kiutendaji sasa  kwa mwaka TTCL  inakusanya shilingi bilioni 212 kutoka shilingi bilioni 102, Bandari imekusanya kutoka shilingi bilioni 703 hadi kufikia shilingi bilioni 838 kwa mwaka, TRC kutoka shilingi bilioni 23 hadi 36 kwa mwaka  na DAWASA shilingi bilioni 32.4 hadi shilingi bilioni 122.4 kwa mwaka ,“ alisema Dkt. Abbasi
Aidha, Dkt. Abbasi alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitatu Serikali ya Rais Magufuli imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta ya  viwanda ambapo jumla ya  viwanda 3,306 viliandikishwa, na vingine vinaendelea kujengwa na baadhi vimekamilika. Halikadhalika viwanda hivyo vimeanza kutengeneza  bidhaa mbalimbali ambapo kati ya hivyo viwanda 251 ni vikubwa na vya kati ni 173.
Ambapo mchango wa ekta ya viwanda katika pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 5.2 mwaka 2015 hadi 5.5 mwaka 2017. Kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda ilikua kutoka asilimia 6.5 mwaka 2015 hadi asilimia 7.1 mwaka 2017/18.
Akiendelea kufafanua mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano Dkt. Abbasi alisema kuwa Rais Magufuli amepambana na rushwa na ufisadi kwa pamoja na mambo mengine, sambamba na  kutimiza ahadi yake ya kuunda Makosa ya Uhujumu Uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi.
“Mpaka sasa kesi mpya 41 zimefunguliwa, na  kuna maombi ya dhamana 346 yamewasilishwa katika Mahakama hii kati ya mwaka  2017 na 2018” alisema Msemaji huyo wa Serikali.
Katika sekta ya usafirishaji nako, Serikali ya Rais Magufuli imefanya mageuzi kadhaa, yaliyopelekea sekta hiyo kupata mafaniko  ya kuwa  na  ndege nne mpya zinazoendelea kuleta mageuzi katika usafiri wa anga nchini, abiria wanaotumia ndege za ATCL wameongezeka kutoka takribani abiria 4,000 kwa mwezi hadi abiria 30,000 kwa mwezi.
Aliongeza kuwa  ndege mbili   aina ya Air Bus zenye uwezo wa kubeba abiria watu 132 zitawasili nchini Disemba mwaka huu, na ndege aina ya  Boeing dreamliner ya pili inatarajiwa kuwasili nchini Oktoba mwaka mwakani.
Aidha, mradi wa umeme wa Stigler’s gorge utakapokamiika unatarajiwa kuzalisha  megawati 2,100, sambamba na mradi wa ujenzi wa reli kwa kiwango cha standarg gauge kutoka Dar es salaam hadi Morogoro na baade Dodoma, ambapo umefikia 33% ya ujenzi.
Mafaniko mengine ya Serikali hii yanaonekana katika katika sekta ya afya,  ikiwemo kujenga vituo vya Afya vya Kata 210 na kukarabati vingine vingi kufikisha idadi ya vituo vinavyotoa huduma hadi mwaka huu kuwa 7,746 kutoka vituo 7,014 mwaka 2014/15 sawa na ongezeko la asilimia 10.4.
 Dkt. Abbasi  alifafanua kuwa vituo hivi pia vina wodi za kina mama na vifaa vya kisasa. Aidha, ajira zaidi ya 6,000 za kada ya afya zimetolewa. Katika miaka mitatu Zahanati zimeongezeka kutoka 6,143 mwaka 2015 hadi 6,646 mwaka huu ikiwa ni sawa na  ongezeko la zahanati 503  ambapo baadhi zilijengwa na zingine kukarabatiwa sawa na ongezeko la asilimia 8.1.
Vilevile, Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mageuzi ya kiutendaji ikiwemo kuongeza Bajeti ya Dawa na Vifaa Tiba kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 2015 hadi kufikia shilingi bilioni 270  kwa mwaka huu wa fedha.
Ongezeko hilo limewezesha upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini kufikia asilimia 89.6 kutoka asilimia 36 mwaka 2015/16. Aidha upatikanaji wa dawa muhimu umepanda kutoka wastani wa asilimia 35 tu hadi asilimia 93.
Sekta ya madini nayo, Dkt. Abbasi alisema kuwa “Serikali iliweka lengo la kukusanya shilingi bilioni 1.5 kwa mwaka kutoka kwa wachimbaji wadogo wa Tanzanite pale Mirerani. Hata hivyo kabla hata ya nusu ya mwaka huu wa bajeti kufika, tayari mapato eneo la Tanzanite yamefikia shilingi milioni 788.5 sawa na asilimia 52 ya lengo la mwaka 2018/19, hii inashadidisha kuwa uamuzi wa Mhe. Rais kujenga ukuta ulikuwa makini,” alisema Dkt. Abbasi
Katika miaka hii mitatu licha ya matukio ya hapa na pale, Tanzania imeendelea, kusimama kama moja ya visiwa vya amani duniani na  Taifa limeendelee kushikamana kawa kuishi kwa amani na upendo.
Aidha, Dkt, Abbasi  alisema kuwa Rais Magufuli anasimamia misingi na Watanzania leo wako huru  kuamua mambo yao kama Taifa, huku akisisitiza  kuwa safari ya kujitegemea imeanza  na mataifa mbalimbali duniani  yanafahamu   azma ya Rais Magufuli kwa Taifa lake.

Comments

Popular posts from this blog

MBINU ZA KUMFIKISHA MWANAMKE MWENYE MAKALIO MAKUBWA KILELENI KWA HARAKA

Kwa kawaida wanawake wanafikia kilele (mwisho wa utamu wa ngono) kati ya dakika ishirini na saa moja, yaani kwa kifupi inawachukua muda mrefu sana hali inayopelekea mpenzi mvivu kuchoka na ufanyaji wake utakuwa wa “ovyo” hali itakayo kufanya wewe kuishiwa na hamu ya kuendelea. Pamoja na kuchelewa huko ambako kunatokana na utofauti wetu kati ya mwanaume na mwanamke lakini nakumbuka hapo nyuma nilikutana na wanawake 2 waliokuwa ndani ya ndoa na wamezaa lakini hawajawahi kabisa kujua utamu wa tendo hilo alimaharufu kama “kufanya mapenzi”. Natambua kuwa ni ngumu au niseme si wanawake wote ambao wamejaaliwa kimaumbile kwamba wanafanikiwa kufika kileleni zaidi ya mara mbili kila wanapofanya mapenzi/ngono (kumbuka ni kati ya dakika 15 na saa moja hivyo Jibaba hapa awe na uwezo wa kujizuia kwa zaidi ya dk 45) na ikiwa jamaa ni “mzamiaji” basi unaweza ukaondoka na goli 3 ktk mzunguuko mmoja. Lakini kwa nini basi baadhi yao tu ndio wafike kileleni na wengine was...

Mushikiwabo to UN: Enhance civilian protection

By Eugene Kwibuka Rwanda’s Minister of Foreign Affairs and Cooperation has urged the United Nations Security Council (UNSC) to invest more energy in the prevention of conflicts for better protection of civilians living in conflict-torn areas. Rwanda’s Foreign minister, Louise Mushikiwabo Louise Mushikiwabo made the call during an open debate on the protection of civilians in armed conflict which the UNSC held in New York on Tuesday. “Rwanda’s core message today is that enhancing the protection of civilians in armed conflict requires action before a conflict starts. The proliferation of non-state armed groups makes civilian protection both more urgent, and harder to achieve,” she said. For better protection of civilians in armed-conflict areas, the minister emphasised the need to increase investments in professionalising the military and police forces through adequate training. “Only when the leadership of armed forces shares the international...

Saudi King urges U.N. action against religious insults

Saudi King Abdullah urged the United Nations to produce a resolution condemning insults on monotheistic religions after the anti-Islam film in the U.S. that sparked deadly protests in many Muslim countries last month. (AFP) By AFP, MINA/SAUDI ARABIA Saudi King Abdullah on Saturday demanded a U.N. resolution condemning insults on monotheistic religions after a low-budget film produced in the U.S. sparked deadly protests last month. “I demand a U.N. resolution that condemns any country or group that insults religions and prophets,” he said during a meeting at his palace with religious figures and heads of hajj delegations in the Mina valley where pilgrims were performing final rituals of hajj. “It is our duty and that of every Muslim to protect Islam and defend the prophets.” A low-budget film produced in the U.S., Innocence of Muslims, triggered a wave of deadly anti-American violence last month across the Muslim world targeting US symbols ranging ...