Msanii wa muziki Diamond Platnumz yupo kwenye mazungumzo na mmoja kati ya wadau wa muziki kutoka Afrika Kusini kwaajili ya kutengeneza ukumbi wa burudani Dar es salaam.
Akizungumza na chanzo kimoja ambacho si blog hii , mmoja kati Wakurugenzi wa Wasafi Festival, Mkubwa Fella amesema tayari Diamond ameshazungumza na mdau huyo kutoka Afrika Kusini na yupo tayari kutumia zaidi ya tsh bilioni 1 kwaajili ya ujenzi wa ukumbi huo mkubwa.
“Baada ya kukutana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa tumemkumbusha tena kwamba kama tutapata uwanja, tunaweza kujenga ukumbi wa burudani, tumepata mwekezaji ambaye yupo tayari kuwekeza zaidi ya tsh bilioni 1,”
Comments