Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni ugonjwa wa kimataifa unaoleta fedheha kubwa katika jamii zote duniani . Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake maalumu kuhusu siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ambayo huadhimishwa kila mwaka Novemba 25.
Guterres amesema ugonjwa huo ni kinyume cha maadili kwa wanawake na wasichana wote, na ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo jumuishi , yaliyo sawa na endelevu. Katika msingi wake, ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni udhihirisho la ukosefu mkubwa wa heshima, kushindwa kwa wanaume kutambua usawa wa asili na utu wa wanawake. Ni suala la haki za msingi za binadamu.
Amekumbusha kwamba ukatili unaweza kuchukua sura yoyote kuanzia ukatili majumbani, hadi usafirishaji haramu wa binadamu, kuanzia ukatili wa kingono katika miozo hadi ndoa za utotoni, ukeketaji na kuuawa.
Ukatili huu unawaumiza watu binafsi na unaathari kubwa kwa familia na jamii kwa ujumla. Guterres ameongeza kuwa “ukatili dhidi ya wanawake unaambatana na masuala mapana ya madaraka na udhibiti katika jamii zetu. Tunaishi katika jamii za mfumo dume na wanawake wanawekwa katika hatari ya ukatili kupitia njia mbalimbali ambazo zinawakosesha usawa.”
Katika mwaka uliopita tumeshuhudia ongezeko la aina moja ya ukatili huu .Unyanyasaji wa kijinsia unawakumba wanawake wengi katika wakati fulani wa maisha yao. Kuongezeka kwa wanawake wengi kupazia sauti zao kuhusu suala hili kutoka katika kila pembe ya dunia na katika kila aina ya maisha , inadhihirisha ukubwa wa tatizo na kudhihirisha nguvu ya nguvu ya harakati za wanawake katika kuchagiza kuchukua hatua hatua na uelimishaji unaohitajika ili kuondokana na unyanyasaji nana ukatili kila mahali.
Katibu Mkuu amesema mwaka huu kampeni ya kimataiga ya Umoja wa Mataifa UNiTE ya kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana inadhihirisha uungaji mono wetu kwa waathirika na wapiga debe wa kupinga ukatili chini ya kaulimbiu “igeuze dunia kuwa rangi ya machungwa : nisikie nami pia au : #HearMetoo,” ikitumia rangi ya chungwa kama rangi ya mshikamano , hasghitag hiyo inalenga kutuma ujumbe byana kwamba :ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni lazima ukomeshwe sasa, na sote tuna jukumu katika hilo.
Guterres amehoji kuwa licha ya kampeni na ufadhili unatotolewa kupambana na ukatili huu si tija hadi pale nusu ya watu wote wanaowakilishwa na wanawake na wasichana wanaweza kuishi huru bila hofu, ukatili na kuhofia usalama wao, hatuwezi kusema, tunaishi katika dunia ambayo ina usawa na haki.
- Get link
- X
- Other Apps
- Get link
- X
- Other Apps
Comments