Nyota wa muziki wa Pop Duniani, Marehemu Michael Jackson ni moja ya wanamuziki wanaoendelea kupiga pesa ndefu
Aliyekuwa msanii nguli wa muziki wa Pop Duniani, Marehemu Michael Jackson ametajwa kuwa ndiye mtu aliyefariki ambaye ameingiza mkwanja mrefu zaidi duniani.
Kwa mujibu wa jarida la Forbes, Michael Jackson ameingiza kiasi cha dola milioni $400 ambacho ni sawa na Tsh. Bilioni 919.
Kwenye orodha hiyo ya majina 13 ya watu waliofariki ambao wameingiza mkwanja mrefu kwa mwaka 2018 (The Highest-Paid Dead Celebrities Of 2018), yupo pia Bob Marley, XXXTentacion na Muhammad Ali.
Highest-Paid Dead Celebrities 2018
1. Michael Jackson ($400 Milion)
2. Elvis Presley ($40 million)
3. Arnold Palmer ($35 million)
4. Charles Schulz ($34 million)
5. Bob Marley ($23 million)
6. Dr. Seuss ($16 million)
7. Hugh Hefner ($15 million)
8. Marilyn Monroe ($14 million)
9. Prince ($13 million)
10. John Lennon ($12 million)
11. XXXTentacion ($11 million)
12. Muhammad Ali ($8 million)
13. Bettie Page ($7 million)
Kwa Michael Jackson anatajwa kuwa huu ni mwaka wa sita mfululizo kuongoza orodha hiyo ya watu waliofariki ambao wanaongoza kwa kulipwa duniani.
Comments