Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania, Taifa Stars imekubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Lesotho kwenye mchezo wa kufuzu AFCON 2019.
Kwa matokeo hayo Taifa Stars inakuwa na alama 5 ikiwa imecheza michezo mitano jambo ambalo itahitajika kushinda dhidi ya Uganda kwenye mchezo wake wa mwisho huku ikiwaombea Cape Verde wenye alama 4 waitandike Lesotho.
Bado matumaini ni madogo kwa Taifa Stars kufuzu kwenda AFCON 2019. Mapema kabla ya mchezo huo Rais Magufuli aliwaomba vijana hao warudi nchini na ushindi lakini ndio hivyo mpaka dakika 90 wamekubali kichapo.
Comments