Joe Cole, aliyekuwa mchezaji wa zamani wa Uingereza, ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 37.
Cole, ambaye amewahi kuzitumikia timu mbalimbali zikiwemo West Ham, Chelsea, Liverpool, Lille, Aston Villa, Coventry City ametangaza
kustaafu leo Novemba 13, akielezea kazi yake ya mpira aliyokuwa
akiifanya kwa nuda wa miaka 20 kama ‘a dream come true.’
Kustaafu
kwake kumekuja mara baada ya kuitumikia timu ya Tampa Bay Rowdies kwa
muda wa miaka miwili na nusu imayoshiriki ligi ya United Soccer League
huko nchini Marekani.
“After
20 years of living my dream, the time has come for me to hang up my
boots…” aliandika hivyo katika kurasa zake za Instagram.
Joe
Cole aliwahi kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uingereza, Mawili ya
FA Cups na kufika hatua ya fainali katika michuano ya Ligi ya Mabingwa
UEFA mwaka 2006.
Comments