Katika harakati za kumkomboa mwanamke kiuchumi na kuachana nadhana ya kuwa tegemezi katika jamii inayowamzunguka.
Taasisi ya Motherhood Tanzania kwa kushirikiana na Evelyn Munisi Foundation wameandaa tamasha litakaloweza kuwakutanisha wanawake wajasiriamali mbalimbali na kuweza kuinuana kiuchumi .
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Taasisi ya Motherhood Tanzania Tina Ndonde amesema tamasha hilo litafanyika Novemba 10 katika viwanja vya Hekima Garden vilivyopo mikocheni na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita .
Pia amesema lengo la tamasha hilo ni kumwinua mwanamke kiuchumi na kuweza kujitegemea mwenyewe kwa kujishughulisha na kazi za ujasiriamali ili mwanamke ainuke kiuchumi.
“ kauli mbiu ya tamasha hilo " Mama shujaa ni mlinzi wa familia, tunajua ukimuinua mama umeinua jamii kwa ujumla na ndio maana tunapambana katika kumkombea mwanamke aweze kujitegemea”amesema
Kwa upande wake mmiliki wa Evelyn Munisi Foundation, evelyn munisi amesema wamejikita hasa katika kuwainua wanawake kwasababu kundi hilo ndio wahanga wakubwa sana kwenye jamii.
“kupia jambo hili tumeweza kufikia sehemu kubwa ya jamii hii ya wanawake wenye shida na tumeweza kufanikiwa kuwainua na kujitegemea wenyewe”
Aidha Evelyn amesema Lengo la Tamasha hilo ni kuwasaidia wajasiriamali wadogo wadogo ambao hawana usajiri wowote kwa kuwasaidia kuwakutanisha na Sido,Tbs,Tfda ambao watahusika kuwashauri wajasiriamali hao nini wafanye ili biashara zao ziwe na ubora huku wakiwaa na lengo la kuwainua mwanamke kiuchumi
Comments