Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Mh Sauda Mtondoo amewasisitiza wakandarasi waliopewa kazi za ujenzi wa miradi ya maendeleo ya Serikali kuhakikisha kuwa wanaimaliza kwa wakati ikiwemo Kituo cha polisi ili kianze mara moja matumizi ya kulinda raia na usalama wao kwa ujumla.
Hayo ameyaeleza wakati akieendelea na ziara yake ya kukagua Miradi ya Maendeleo katika Wilaya ya Kilindi akiwa ameongozana na Viongozi mbalimbali katika Tarafa ya Kimbe ambapo amekagua Ujenzi wa Kituo Cha Polisi kinachojengwa ndani ya kata hiyo.
Aidha Mh. Mtondoo ameweza kutembelea na Kukagua pia ujenzi wa Kituo Cha Afya pamoja na madarasa katika Shule ya Tegemezi pamoja na Vyoo.
Hata hivyo Mh Sauda pamoja na msafara wake walimalizia kufanya ziara katika mashamba ya mihogo yaliyo ndani ya Tarafa ya Kimbe na kuwahamasisha wakulima kuendeleza kilomo hicho pamoja na kuwahakikishia uhakika wa soko la mazao yao.
Comments