TIC:Kila taasisi zinapaswa kufanya marekebisho katika utendaji wao ili kusaidia kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)kimesema licha ya uwekezaji kupungua duniani,lakini Tanzania ni miongoni mwa nchi tano duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa.
Ili kuendelea kupiga hatua katika uwekezaji kila taasisi zinapaswa kufanya marekebisho katika utendaji wao ili kusaidia kutengeneza mazingira rafiki kwa wawekezaji.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Bw. Geoffrey Mwambe amesema taasisi za Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wametakiwa kuwa na ushirikiano katika kufanikisha mipango ya uwekezaji hapa nchini jambo ambalo litasaidia taifa kupiga hatua katika sekta ya uchumi.
Amesema taarifa ya Mkutano wa Uwekazaji duniani uliofanyika hivi karibuni nchini Uswiswi, ripoti ya mwaka wa jana inaonyesha uwekezaji duniani umeshuka kwa asilimia 23 kutokana vita ya maneno kati ya nchi ya Marekani na China.
"kutokana na hali hiyo kila nchi duniani inaendelea kutafuta wawekezaji ili kuhakikisha wanapiga hatua uchum,"alisema Mwambe.
Bw. Mwambe alisema kuwa ili kuendelea na kasi hiyo serikali inaendelea na mipango ya kutengeneza uchumi wa mazingira katika masoko, huku sekta binafsi zinapaswa kufanya uwekezaji kwa kuzalisha bidhaa.
Amesema kuwa wakati umefika wa kufanya uwekezaji, huku akizitaka mamlaka husika kuangalia namna kuwapa adhabu wafanyabiasha wanaokwenya kinyume na taratibu ili waendelee kufanya biashara zao.
"Tusifungwe na taratibu zetu za kazi, kama nafasi ipo ya kumsaidia mfanyabiashara tumsaidie ili aendelea kufanya biashara kwa maendeleo ya taifa" amesema Bw. Mwambe.
Hatua hivyo Bw. Mwambe amezitaka sekta binafsi kuwa na umoja katika kufanikisha shughuli za uwekezaji sio kusema maneno ambayo sio rafiki katika kujenga uchumi.
Bw. Mwambe amefafanua kuwa bado kuna maitaji mengi yanaitajika ili kuwavutia wawekezaji katika maeneo hapa nchini.
"Kuna vituo vingi vya utalii hapa nchini ambavyo vinaitaji wawekezaji kupeleka maitaji maeneo mbalimbali ikiwemo kujenga hotel za kisasa" amesema Bw. Mwambe.
Amesema kuwa tunatakiwa kubadilika katika utendaji wa kazi, huku akisisita kuwa kama kuna mtu au kiongozi yoyote anatumika kukwamisha maendeleo kwa wafanyabiashara jina lake litapeleka kwa Mhe. Rais Dkt. John Magufuli" amesema Bw. Mwambe.
Katika hatua nyingine tayari Wajumbe kutoka Jimbo la Dongon,Gwazu Nchini China wamekuja nchini kufanya uwekezaji katika sekta ya viwanda kwenye eneo la Mlandizi mkoani pwani ambapo watawekeza kwenye ujenzi wa viwanda vitatu .
Mkurugenzi wa Uhamasishaji na Uwekezaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC John Mnali aliupokea ujumbe huo wa wawekezaji hao ambapo alisema wamekuja kufanya uwezaji kwenye kiwanda cha kuongeza thamani ya ngozi, kiwanda cha kuteneza saa pamoja na simu ambapo thamani yake kwa awamu ya kwanza ni dola milioni 100.
Mnali amesema kuwa kiwanda cha kuongeza thamani ya ngozi kitatumika kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo viatu,mikanda, pamoja na mikoba ya kimama, huku akiziomba taasisi zinahusika na utoaji wa leseni na vibali kutoa kwa wakati ili uwekezaji ufanyike kwa haraka.
“kazi ya uwekezaji si rahisi tushirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha uwekezaji unafanyika na uwekezji si maneno uwekezaji ni vitendo,” amesema Mnali.
kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni za Kiluwa, Mohamed Kiluwa amesema waliamua kwenda nje kutafuta wawekezaji kuja kuwekeza nchini ili kukuza uchumi wa kati wa viwanda.
Hata hivyo Kiluwa amesema tayari ameshawagusia wawekezaji hao suala la kuwekeza kwenye zao la korosho na atatarajia kwenda nje kukutana na bodi ya wawekezaji hao ili kuweza kuzungumzia suala hilo.
Comments