Wahitimu wa Mafunzo Michezo ya Ngumi na Mpira wa wavu wa majeshi watakiwa kuyatumia mafunzo kwa vitendo.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Majeshi nchini, Brigedia Jenerali Suleimani Mzee wakati akifunga Mafunzo ya Siku 10 yaliyotolewa kwa Wakufunzi wa majeshi wa michezo hiyo pamoja na raia.
Amesema kuwa wakufunzi wote na raia walioshiriki wanatakiwa kuyatuma mafunzo hayo kwa vitendo na sio kuviweka makabatini vyeti vya uhitimu walivyovipata huku akiwahimiza kuyafikisha kwa wananafunzi na raia.
“Umuhimu wa mafunzo mmeuona msifungie vyeti vya mafunzo mliyopewa yatumieni kwa vitendo haitakuwa haina maana yatumieni kuendeleza vipaji vyenu na kuwapa wanafunzi wenu la sivyo mtakuwa mmepoteza muda wenu,” amesesma .
Amebainisha kuwa Tanzania ni mwanachama wa Shirikisho la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) hivyo kupitia uongozi wa jeshi na ubalozi waliomba kupatiwa wakufunzi kutoka nchi hiyo na kufanikiwa kuwapata na kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kuwajengea uwezo na kuendeleza vipaji.
Amesisitiza kuwa mafunzo hayo yalishirikisha jumla ya wakufunzi 56 kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania, jeshi la Polisi, Jeshi la Zima Moto na Uokoaji na raia na kubainisha yalitolewa na wakufunzi wanne kutoka Jeshi la Ujerumani.
Amefafanua kuwa endapo mafunzo waliyoyapata hawatayazingatia watakuwa wamewapotezea muda wakufunzi waliokubali kuja nchini kuwaongezea ujuzi wao.
Brigedia Jernerali Mzee amesema kwa kuwa mafunzo hayo yana umuhimu wanaangalia uwezekano wa kufanyika awamu ya pili ya mafunzo hayo mwakani.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utimamu wa mwili, michezo na utamaduni, Kanali Erasimus Bwegoge amesema mafunzo hayo yatasaidia kuinua michezo hiyo pamoja na kuwasaidia makocha kuwaongezea ujuzi makocha wote walioshiriki.
Naye Mkufunzi Mkuu wa mafunzo hayo, Kapteni Paul Klar kutoka jeshi la ujerumani ,amefurahishwa na ukarimu na ushirikiano waliopewa na washiriki katika muda wote wa mafunzo na kusisitiza kuwa wamejifunza kwa ujumla maisha ya watanzania.
Kapteni Klar amesema washiriki walikuwa wakiyapokea vizuri na kwamba watapohitajika kwa mara nyingine watakuwa tayari kuja nchini.
Mwisho.
Comments