Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya CUF, Abdallah Mtolea ametangaza rasmi kujivua uanachama wa chama hicho pamoja na kuachia nafasi yake ya Ubunge kuanzia leo.
Mtolea ametangaza uamuzi huo bungeni jijini Dodoma mapema leo Novemba 15, 2018 kwenye mkutano wa 13 kikao cha 8 kinachoendelea Jijini humo na kueleza sababu kuwa hakuna maelewano ndani ya chama hicho.
Hata hivyo, hajatoa tamko kuwa atajiunga chama gani? ingawaje amevikaribisha vyama vingine vya kisiasa kuwa yupo tayari kujiunga navyo endapo vitamkubalia.
Maamuzi hayo yamekuja ikiwa leo ndio tarehe ya mwisho iliyowekwa na CCM kwa viongozi wa vyama vingine wanaotaka kuhamia ndani ya chama hicho, na kupewa dhamana ya kutetea udiwani au Ubunge wao.
Comments