Timu ya Taifa ya Nigeri ‘The Super Eagles’ hapo jana siku ya Jumanne ilikuwa na kibarua kizito cha kukabiliana na Uganda ‘the Cranes’ kwenye mchezo wa kirafiki uliyopigwa katika dimba la Stephen Keshi.
Kwenye mchezo huo uliyopigwa Novemba 20, mshambuliaji wa Uganda na klabu ya Simba, Emmanuel Okwi alikutana na nyota wa Nigeria na timu ya Arsenal, Alexander Iwobi ambapo walipata nafasi ya kusalimiana na kupiga picha ya pamoja.
Picha ya wawili hao imezua mihemko tofauti kwa baadhi ya watu, wengine wakiamini kuwa katika hali ya masihara tu Okwi anaweza kujipatia nafasi katika klabu moja wapo nchini Uingereza kutokana ukaribu uliyoonekana kati yake na Iwobi.
Katika mechi hiyo ya kirafiki Nigeria ilitoka sare tasa ya bila kufungana 0 – 0 dhidi ya Uganda ambayo inakabiliwa na mchezo na Tanzania Machi 22 kukata tiketi ya kufuzu Afcon mwakani.
Nigeria imeshajikatia tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon mwaka 2019 baada ya kutoka sare ya 1 – 1 na timu ya taifa ya Afrika Kusini mchezo uliyopigwa Johannesburg.
Kwa upande wa Uganda nayo imeshajikatia tiketi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa baada ya kuifunga Cape Verde ba 1 – 0 mchezo uliyopigwa uwanja wa Nelson Mandela jijini Kampala.
Kikosi cha Super Eagles XI vs Uganda: Akpeyi; Ogu, Ajayi, Idowu, Collins; Etebo, Mikel Agu, Iwobi; Chukwueze, Osimhen, Musa (c).
Kikosi cha Uganda XI vs Nigeria: Salim Jamal, Nico Wadada, Godfrey Walusimbi, Dennis Iguma, Timothy Denis Awanyi, Khalid Aucho, Tadeo Lwanga, Emmanuel Arnold Okwi, Moses Waiswa, Allan Kyambadde, Derrick Nsibambi.
Comments