WAKAZI wa Mbagara Kuu n a viunga vyake wapo
hatarini kuugua magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosekana kwa maji safi na
salama takribani miezi tisa.
Wakazi hao waliliambia gazeti hili kuwa adha hiyo ya
upatikanaji wa maji imetokana na ujenzi wa Barabara zinazo boreshwa kwa kiwango
cha lami katika mitaa ya Kata ya Mbagara kuu iliyo sababisha uharibifu wa
miundo mbinu.
Blog hii ililifanya
jitihada mahususi ili kupata maelezo ya kina kutoka kwa Kampuni zinazotekeleza
ujenzi wa barabara hiyo ambazo ni Group six kutoka China na Harrising kutoka
India lakini hawakupatikana.
Kutokana na kutopatikana kwa wahusika wa Kampuni hizo mbili
ambazo zinawajibika kurejesha miundo mbinu ya maji katika utaratibu wa kawaida
na shughuli za ujenzi wa barabara ukiendelea Blog lilizungumza na Diwani wa
kata hiyo Shaban Abubakari.
Abubakari alikiri kuwepo kwa tatizo la upatikanaji wa maji
katika mitaa ya Kata ya Mbagara Kuu ikiwemo Mbagara Kuu Magharibi, Kusini na
Mgeni nani Kijichi ambapo barabara 11 za mitaa hiyo zinatengenezwa kwa kiwango
cha lami.
“Kutokana na wananchi wangu kuathiriwa na adha ya maji, nimeiamuru Kamati ya Maji kuhakikisha
Wakandarasi wanarekebisha miundombinu ya maji inarejea katika hali ya kawaida
kama ilivyo kuwa awali nanimetoa wiki
moja ifikapo jumatatu ya juma hili mkandarasi awe amekwisha anza utekelezaji na
baadhi ya mitaa ipate maji,”amesema
Agizo hilo lililotolewa mwishoni mwa juma na hadi kufikia
jana halikuweza kufanikiwa ilhali wakandarasi hao na Mwenyekiti wa Kamati ya
maji wakisema Mkandarasi wa maji alikwisha patikana.
Blog ilifanya jitihada za kumtafuta mkandarasi huyo bila
mafanikio ambapo simu yake iliita bila kupokelewa, hata hivyo Diwani Abubakari
alisema ifikapo Ijumaa hii kama hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kuhusu
upatikanaji wa maji hatua zaidi zitachukuliwa dhidi ya wakandarasi hao.
Naye Mtendaji wa Kata hiyo Rajab Ramadhani, alisema kabla ya
ukarabati wa barabara za mitaa ya kata hiyo hakukuwa na tatizo la upatikanaji
wa maji kwakuwa upo mradi wa maji unaosimamiwa na serikali ya mtaa huo ambao
ulikuwa ukikidhi mahitaji ya msingi ya wananchi wa maeneo hayo.
“Hadi ifikapo ijumaa hii (leo) tatizo hili litapatiwa
ufumbuzi wanaoathirika si wananchi pekee, hata sisi ni wahanga wa tatizo hili
hivyo wavute subira ili suluhisho la tatizo hili lipatikane,”amesema.
Habiba Said mkazi wa mtaa wa Mgeninani alisema afya zao zipo
hatarini kwa magonjwa ya mlipuko hususani kipindi hiki cha vuli ambapo mvua
nyingi zitanyesha na kuzoa taka nyingi kutoka mitaani na kuingia katika mito
wanayoitegemea na taka hizo zitakuwa na mkusanyiko wa kinyesi.
Dumu moja la lita 20 za maji huuzwa kati ya shilingi 500-700
ilihali maji hayo usalama wake unatiliwa mashaka kwakuwa watumiaji hawana
uhakika na vyanzo vya maji wanayo nunua mtaani.
Comments