Waziri wa Kilimo nchini Josephat Hasunga awataka wakulima nchini kuongeza thamani ya mazao ya kilimo
WAZIRI wa Kilimo Josephat Hasunga amewataka wakulima nchini kuongeza thamani ya
mazao ya kilimo ili wakulima hao
wanufaike zaidi.
Ushauri huo ulitolewa na Waziri Hasunga jana alipo wahutubia
wadau sekta binafsi ya kilimo nchini katika mkutano wa wadau hao uliofanyika
Jijijini Dar es Salaam.
“Ni wakati wawakulima
wetu kubadilika kwakuongeza thamani ya bidha ili kuhimili ushindani wa soko
lakini hata kupata faida zaidi ,wakulima wetu wakifundishwa kusindika bidhaa
zenye ubora kwakuzingatia usalama wa chakula tunaamini tutaleta mapinduzi ya
sekta ya kilimo nchini,” amesema Hasunga.
Hasunga alisema serikali kwakushirikiana na sekta binafsi
wanayo mipango mingi ya kuboresha sekta ya kiliomo ambayo ndiyo sekta yenye
mchango mkubwa kuliko sekta zote nchini.
Aidha Hasunga amesema hali ya hakiba ya chakula nchini ni ya
kuridhisha zaidi ambapo kwa mwaka huu kuna uzalishaji wa chakula kwa asilimia
125 na vikwazo mbalimbali ikiwemo utitiri ushuru ukiwa umeondolewa.
Hasunga aliwaambia wadau hao na wakulima kwa ujumla kuwa
Biashara ya kuuza mazao nje ya nchi imefunguliwa na wakulima wana uwezo wa
kuuza mazao yao nje ya nchi.
Kuhusu ununuzi wa korosho unaoendelea katika mikoa ya kusini
Waziri Hasunga alisema wakulima hao wanaendelea kulipwa na alisema kuwa Korosho
zitakazo pelekwa sokoni zote zitakuwa zimebanguliwa hazitauzwa kama korosho
ghafi.
Abala Ulega mkulima kutoka Namtumbo aliliambia gazeti hili
kuwa serikali iliangalie upya suala la mbolea
na pembejeo kwakuwa hakuna bei elekezi na kumekuwa na mfumuko wa bei
usio zingatia hali za wakulima.
“Serikali itoe bei elekezi kwa pembejeo nchini kwakuwa
wananchi wanataabika na wengi kipato chetu ni duni,serikali ikitoa tamko la bei
elekezi itakuwa imemsaidia mkulima”amesema
Comments