Katika
droo ya michuano ya klabu barani Afrika iliyotajwa na Shirikisho la
Soka Afrika (CAF), wawakilishi wa Zanzibar, JKU watamenyana na Al Hilal
ya Sudan na mshindi baina yao atakutanana mshindi kati ya APR FC ya
Rwanda na Club Africain ya Tunisia.
mechi
za kwanza za raundi ya pili ya pili na ya mwisho ya mchujo zitachezwa
kati ya Desemba 14 na 16 na marudiano Desemba 21 na 23, mwaka huu.
Katika
Kombe la Shirikisho, Mtibwa Sugar itaanza na Northern Dynamo ya
Shelisheli na ikivuka mtihani huo itakutana na K.C.C.A ya Uganda.
Wawakilishi
wa Zanzibar, Zimamoto wamepewa kigongo, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini
na mshindi baina yao atakutana na mshindi kati ya El Geco ya Madagascar
na Deportivo Unidad ya Equatorial Guinea.
Comments