Kocha wa timu ya taifa ya Misri, Javier Aguirre amemtaka nyota wake Mo Salah kuwachana na klabu ya Liverpool kama meneja wa klabu hiyo Jurgen Klopp atashindwa kutwaa taji msimu huu.
Salah ambaye amefunga jumla ya mabao 44 msimu uliyopita amejikuta akiingia kwenye majeraha makubwa katika mchezo wa fainali ya Champions League walipokuwa wakiikabili Real Madrid.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha The Sun, Aguirre amemtaka meneja Jurgen Klopp kuhakikisha anatwaa taji msimu huu kama anahitaji kuendelea kuwa na nyota huyo tegemezi wa Misri.
Miamba ya soka ya Hispania Real Madrid imekuwa ikimtolea macho Salah kwa muda mrefu katika kunasa saini yake ili kuziba pengo la Cristiano Ronaldo.
Licha ya kuwa Liverpool imetwaa mataji mawili tangu mwaka 2006, Aguirre amesema kuwa Salah yupo Anfield kwaajili ya kushinda mataji makubwa hivyo ni lazima kuangalia mbali zaidi kama yanashindikana. Hivyo ni vema kuachana na Liver kama ndani ya misimu huu itashindwa kutwaa mataji.
Comments