Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2013

Alicia Keys 'Brand New Me' Part II + She Appreciate The Overwhelming Support From The Fans!! -- Track Inside

Posted by Futuristic Blogger   Alicia Keys 'Brand New Me' Part II  + She Appreciate The Overwhelming Support From The Fans And Happy Birthday Wishes!! -- Track Inside -- Alicia Keys 'Brand New Me' Part II  + She Appreciate The Overwhelming Support from The… Continue

HII NDIYO CAPE VERDE

PORT ELIZABETH, Afrika Kusini HUWEZI kuamini, lakini ndivyo ilivyokuwa. Cape Verde juzi ilionyesha maajabu baada ya kuichapa Angola mabao 2-1 na kufuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika. Katika mechi hiyo ya kundi A iliyochezwa mjini hapa, Angola ilikuwa ikihitaji ushindi ili iweze kufuzu kucheza hatua hiyo na ilikuwa ya kwanza kupata bao. Mlinzi Neves wa Cape Verde ndiye aliyeizawadia bao Angola dakika ya 33 baada ya kujifunga wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira wa hatari uliopigwa kwenye lango la timu yake. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko. Cape Verde ilisawazisha dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika kwa bao lililofungwa na beki, Fernando Varela kwa shuti la umbali wa mita zipatazo 17. Wakati mashabiki wakiamini kuwa pambano hilo lingemalizika kwa sare, Heldon aliifungia Cape Verde bao la pili na la ushindi na kuwafanya wachezaji na viongozi wa timu hiyo wapagawe kwa ushindi. Angola ililianza pambano hilo kwa kasi, k

Lebron James And The Miami Heat Visits The White House,Plus Gives Obama His Own Jersey-Video Inside!

Posted by  DADDYMACK   Lebron James And The Miami Heat Visits The White House,Plus Gives Obama His Own Jersey-Details & Video Inside!Lebron James And The Miami Heat Visits The White House,Plus Gives Obama His Own Jersey-Details & Video… Continue

Wendy Williams The New Oprah Winfrey Of Daytime Television?? Details & Video Inside!

Posted by DADDYMACK   No one can deny that the the 48 gossip-holic has took daytime TV by storm with hit show "The Wendy Williams Show" The ratings are through the roof and big wigs are after her for another season.  Bloomberg Television caught… Continue

Rick Ross 2013 Birthday Weekend Right BEFORE The Drive By Shooting. Rozay Shuts Down Club Liv and Compound!! - Video Inside

Posted by Futuristic Blogger   Rick Ross 2013 Birthday Weekend Right Before The Drive By Shooting. Rozay Shuts Down Club Liv and Compound!! - Rick Ross 2013 Birthday Weekend Right Before The Drive By Shooting. Rozay Shuts Down Club Liv and Compound!! - Video Inside Rick Ross 2013 Birthday Weekend Right Before The Drive By Shooting. Rozay Shuts Down Club Liv and Compound!! - Video Inside Rick Ross 2013 Birthday Weekend Right Before The Drive By Shooting. Rozay Shuts Down Club Liv and Compound!! - Video Inside Rick Ross 2013 Birthday Weekend Right Before The Drive By Shooting. Rozay Shuts Down Club Liv and Compound!! - Video InsideSource

Wahisani waahidi Dola milioni 600 kusaidia vita vinavyoendelea Kaskazini mwa Mali kukabiliana na magaidi

Na Nurdin Selemani Ramadhani Mkutano wa Kimataifa uliowaleta pamoja Viongozi wa nchi za Afrika na Maofisa wa Kimataifa umefanikiwa kukusanya jumla ya dola milioni 600 kwa ajili kusaidia vita vinavyoendelea Kaskazini mwa Mali. Wanajeshi wa Ufaransa wakiwa katika Mji wa Timbuktu baada ya kuuchukua kutoka kwa Makundi ya Kiislam. REUTERS/Arnaud Roine/ECPAD/Handout Wafadhili mbalimbali wamechangia fedha kwa ajili ya kuendeleza vita iliyopewa jina Vita ya Kupambana na Ugaidi Kaskazini mwa Mali lengo likiwa ni kuyasambaratisha Makundi ya Kiislam yaliyokuwa yanatawala kwa miezi zaidi ya tisa. Mkutano huo umefanyika nchini Ethiopia ambapo mataifa hayo yameahidi pia kuchangia kijeshi ili kufanikisha kukabiliana na vitendo vya kigaidi ambavyo vyanzo vyake vimekuwa vikitanjwa kuwa nchini Mali. Japan imechangia dola milioni 120 huku Marekani ikitoa kitita cha dola milioni 96 kati ya dola milioni 600 ambazo zimeahidiwa kutoka kwa nchi ambazo zimehudhur

HATIMAYE LULU APATA DHAMANA, ASEMA 'NIOMBEENI, SAFARI NDEFU'

NA FURAHA OMARY WA GAZETI LA UHURU “WATU waendelee kuniombea, hii ni dhamana tu, lakini kesi bado, safari ni ndefu. Namshukuru Mungu, yeye ndiye kila kitu.” Hiyo ni kauli ilitolewa na msanii wa maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, baada ya kuachiwa kwa dhamana na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, katika kesi inayomkabili ya kuua bila kukusudia. Lulu, ambaye alikuwa anasota rumande kwa takriban miezi minane katika gereza la Segerea, kuanzia Aprili mwaka jana, anashitakiwa kwa kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba. Msanii huyo aliachiwa huru kwa dhamana jana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu wa Kanda hiyo, Francis Kabwe baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa juzi na Jaji Zainabu Mruke wa mahakama hiyo. Akizunguzumza na waandishi wa habari baada ya kutoka nje ya jengo la Mahakama Kuu, Lulu alisema anawashukuru watu wote na kuwaomba waendelee kumuombea kwa kuwa hiyo ni dhamana tu,kesi bado inaendelea na safari n

VICTORIA AIBUKA NA TAJI AUSTRALIA OPEN

MELBOURNE, Australia VICTORIA Azarenka wa Belarus jana alifanikiwa kutetea taji lake la ubingwa wa michuano ya wazi ya tennis ya Australia kwa wanawake baada ya kumbwaga Li Na wa China. Katika mechi hiyo ya fainali, iliyokuwa na msisimko wa aina yake, Victoria alimshinda Li Na kwa seti 2-1. Li Na aliianza seti ya kwanza kwa kishindo na kumbwaga Victoria kwa 6-4. Lakini mwanadada huyo wa Belarus alichachamaa katika seti mbili zilizofuata na kushinda kwa 6-4, 6-3. Kabla ya mchezo huo, Victoria alikuwa hapewi nafasi kubwa ya kutwaa tena taji hilo. Baadhi ya magazeti ya Australia na hata wasomaji wake, walikuwa wakitoa nafasi kubwa kwa Li Na kuibuka mshindi kutokana na uwezo aliouonyesha katika mechi za hatua ya awali. Mara baada ya pambano hilo kumalizika, Victoria alijikuta akikaa kwenye kiti uwanjani na kuanza kuangua kilio. Alilazimika kutumia taulo kufuta machozi yake. Victoria ndiye mchezaji namba moja duniani kwa sasa katika mchezo huo kwa wanawake.

Kinana: Serikali iwasikilize wananchi wa Mtwara

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,  Abdulrahman Kinana SAKATA la gesi sasa limeingia hatua mpya, baada ya watendaji wakuu wa CCM; Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kuitaka Serikali ikae na wana-Mtwara ili kuona namna ya kumaliza mgogoro huo kwa amani. Kinana na Nape walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti jana. Wakati Kinana alisema hayo alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara mkoani Kigoma, Nape alifanya hivyo kupitia mtandaowa Twitter na baadaye kuthibitisha kauli hiyo alipoulizwa na mwandishi wetu. Wakati watendaji hao wa CCM wakitoa matamko hayo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda jana alifanya vikao mfululizo mkoani Mtwara akisaka suluhu ya mgogoro huo. Kinana na Nape Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Uvinza, Kigoma, Kinana aliitaka Serikali isikilize hoja za wakazi wa Mtwara na kuzitafutia usumbufu sahihi. Mbali na kutoa ushauri huo, aliitaka

Majeshi ya Ufaransa na Mali yaendelea na doria katika Mji wa Timbuktu

Majeshi ya Ufaransa na Mali yanaendelea kufanya doria katika Mji uliojaaliwa misitu mingi wa Timbuktu baada ya kupata mapokezi ya kishujaa kutoka kwa wakazi wake baada ya Makundi ya Kiislam ambayo yalikuwa yameweka makazi yao kwa kipindi cha miezi tisa kuondoka. Msikiti uliopo katika Mji wa Timbuktu, Mali eneo ambalo limechukuliwa na Majeshi ya Ufaransa na Mali Doria hii ni harakati za kufanya uchunguzi kama Wapiganaji wa Makundi ya Kiislam wameendelea kujihifadhi katika maeneo mbalimbali kwenye Mji wa Timbuktu baada ya kuingia kwenye eneo hilo bila ya kukabiliwa na upinzani wa aina yoyote. Wananchi wa Mji wa Timbuktu wameonesha furaha yao pindi tu majeshi ya Ufaransa na yale ya Mali yalipofanikiwa kuingia katika Mji huo ikiwa ni ishara ya kuurejesha tena kwenye mikono ya serikali baada ya kuanguka kwa wapiganaji hao. Wakazi wa timbuktu wamewapokea wanajeshi wa Ufaransa na Mali kama mashujaa huku wakiimba “Mali, Mali, Mali” na kupeperusha bendera za

US senators plan immigration reform

A bipartisan group of US senators has unveiled a plan for sweeping reform of the immigration system this year. Senator John McCain: “What has been created is a de facto amnesty” The framework calls for a path to citizenship for many of the 11 million undocumented immigrants in the US, while tightening border security. The eight senators promoted their proposals a day before President Barack Obama presents his own blueprint. Correspondents say conservatives’ hard line on immigration has become an electoral liability for Republicans. In last November’s elections, President Obama, a Democrat, won more than 70% of the Hispanic vote. ‘Time is right’ Senator Charles Schumer of New York told Monday’s news conference he hoped the bipartisan group’s blueprint could pass the Senate by late spring or summer. But many conservative lawmakers denounce a path to legalisation for undocumented immigrants as an “amnesty” for lawbreakers. Read more »

Serikali ya Somalia Kufanya Mfumo wa mishahara kuwa wa kisasa

Na Adnan Hussein, Mogadishu Serikali ya Somalia itaanzisha mpango mpya hapo Aprili wa kuwalipa waajiriwa wake kupitia mfumo wa automatiki unaodhibitiwa na Benki Kuu ya Somalia. Mfumo mpya katika mwezi wa Aprili utaanza kutumiwa kuwalipa waajiriwa wa serikali, ikiwa ni pamoja na wajumbe hawa wa Kikosi cha Polisi ya Somalia, moja kwa moja kupitia Benki Kuu ya Somalia. [Na AFP Photo/AU-UN IST Photo/Stuart Price] Waziri wa Fedha na Mipango Mohamud Hassan Suleiman aliiambia Sabahi kuwa programu hiyo ni moja miongoni mwa mipango kadhaa yenye lengo la kuufanya mfumo wa fedha nchini kuwa wa kisasa, kutoa uwiano wa bajeti na kuzuia ufisadi wa kitawala na kifedha. Waajiriwa wa serikali kwa sasa wanalipwa fedha taslimu na wahasibu waliopangiwa katika wizara zao husika baada ya fedha kulipwa na Benki Kuu. Wahasibu ndio wenye dhamana ya kukusanya fedah na kumlipa kila mwajiriwa baada ya kutia saini risiti ya karatasi kama njia ya uthibitisho. Mchakato h

CHADEMA yapanga mikakati ya urais 2015

Na Ratifa Baranyikwa KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imekutana katika kikao maalumu kutafakari na kupanga mikakati katika mambo makuu manne, likiwamo la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2014/2015. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Blue Pearl, ambako kikao hicho kinaendelea leo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, alisema wameamua kujifungia na kupanga mikakati ya Uchaguzi wa Serikali na Mitaa mwaka 2014 na ule Mkuu wa mwaka 2015 ili kujiweka sawa. Hatua hiyo ya CHADEMA imekuja wakati ambapo vita ya urais imeendelea kushamiri ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku vigogo wanaotajwa kuwania nafasi hiyo nao wakionekana kujipanga na kuandaa mikakati kuelekea mwaka 2015. CHADEMA kinaonekana kuwa ndicho chama pekee cha upinzani ambacho kimejizolea umaarufu mkubwa kwenye medani ya siasa katika miaka ya hivi karibuni, kikichukua nafasi iliyokuwa imekaliwa na Ch

BAFANA BAFANA WAINGIA ROBO FAINALI

DURBAN, Afrika Kusini WENYEJI Afrika Kusini, maarufu kwa jina la Bafana Bafana, juzi walifuzu kucheza robo fainali ya michuano ya soka ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 na Morocco. Sare hiyo iliiwezesha Bafana Bafana kutwaa uongozi wa kundi A ikiwa na pointi tano baada ya kucheza mechi tatu, sawa na Cape Verde, lakini zinatofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa. Morocco, ambayo ilitakiwa kushinda pambano hilo ili isonge mbele, iliweza kuwa mbele kwa mabao mara mbili, lakini mara zote Bafana Bafana ilisawazisha. Issam El Adoua aliifungia Morocco bao la kuongoza dakika ya 10 baada ya kioa Itumeleleng Khune wa Bafana Bafana kuokoa vibaya mpira wa kona, ukamkuta mfungaji aliyeunganisha wavuni. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko. May Mahlangu aliisawazishia Bafana Bafana dakika ya 71 na kuamsha shamra shamra kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo. Mehdi Namli aliiongezea Morocco bao la pili dakika ya 81 kabla ya Siyabonga Sangweni kuisa

LULU AKIWA MAHAKAMA KUU LEO

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, imetoa masharti ya dhamana kwa msanii wa maigizo nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba. Hata hivyo, Lulu ambaye alikuwa na uso wa furaha jana baada ya kutolewa kwa masharti hayo, alirudishwa rumande kutokana na kutokuwepo kwa Msajili wa Mahakama Kuu wa kanda hiyo, kwa ajili ya kuhakiki iwapo masharti yaliyotolewa na Jaji Zainabu Mruke yametimizwa. Masharti hayo ya dhamana ni kwamba, muombaji (Lulu) awasilishe hati zake zote za kusafiria kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, asisafiri nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ya idhini ya msajili, kuripoti kwa msajili kila tarehe moja ya kila mwezi tangu atakapotimiza masharti hadi shauri litakapomalizika. Masharti mengine ni Lulu awe na wadhamini wawili watakaotia saini bondi ya sh. milioni 20 kila mmoja na wawe wafanyakazi wa serikali na Msajili wa Mahakama Kuu wa Kanda hiyo, ataha

Signing Exchange of Notes:

  Hon. Dr. William A. Mgimwa, Minister for Finance, (left) and H. E. Mr. Masaki Okada, Ambassador of Japan (right) signing the Exchange of Notes Hon. Dr. William A. Mgimwa, Minister for Finance, addressing the media after the signing of the Exchange of Notes .

Jennifer Lopez

Jennifer Lopez's bikini body makes a splash in Miami

Fitness book, ‘Formula 50,’

Richard Corkery /New York Daily News Curtis '50 Cent' Jackson signs copies of his new fitness book, 'Formula 50'' at a Manhattan Barnes and Noble earlier this month. Related Stories Manny Pacquiao in talks with rapper 50 Cent about business relationship as much talked about fight with Floyd Mayweather Jr. remains unlikely  Rapper 50 Cent is suing over loan to makers of Sleek by 50 headphones for $346,429 50

Nigerian Musician

Sexy Nigerian musician Aituaje Iruobe, widely known as WAJE.

Karibu Leo Kinyerezi Katika Babata za 'Kufamtu'

 The blue Point  na wadau mbli mbli inakuletea  .... Ile siku imewadia na punde imefika  ile siku yenye shughuli  nzito na yakipekee yaani nyama choma huku tukiangalia dunia kupitia Dstv ni jumapili ya leo  kuanzia  12 :00 mchana hadi Jooni ya saa 5:00 usiku  hInshu hii nafanyika Kinyerezi Mwisho

KIMBEMBE JANA SIMBA, AZAM, COASTAL UNION ZAUA

MABINGWA watetezi Simba leo wameuanza vyema mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya kuichapa African Lyon mabao 3-1 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika pambano hilo, Simba ingeweza kutoka uwanjani na ushindi mkubwa wa mabao iwapo mshambuliaji wake, Mrisho Ngasa angekuwa makini kila alipolifikia lango la African Lyon. Ngasa pia alipoteza penalti katika kipindi cha pili baada ya shuti lake kumlenga kipa Abdul Seif. Hadi mapumziko, Simba ilikuwa mbele kwa mabao 3-0. Mabao ya Simba katika kipindi hicho cha kwanza yalifungwa na Mrisho Ngasa, aliyefunga mawili na Ramadhani Chombo 'Redondo'. Redondo, aliyerejea Simba akitokea Azam, alifunga bao la kwanza dakika ya tatu baada ya kuunganisha wavuni mpira wa krosi uliopigwa na Ngasa kutoka pembeni ya uwanja na kuamsha shangwe kutoka kwa mashabiki wa Simba. Bao la pili lilifungwa na Ngasa baada ya gonga safi kati yake na Mwinyi Kazimoto kabla ya kufumua shuti l

VURUGU TUPU TANZANIA

Vijana wakazi wa Dumila na vitongo vyake wakiangusha gari aina ya Land Cruizer T 241 AMS mali ya mfugaji katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro wakati wa vurugu zilizodumu kwa masaa sita kwa kuweka vizuwizi kwa lengo la kumshinikiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdera kusikiliza kero za wakulima.Picha na Juma Mtanda  MWANANCHI Mkoani Mororgoro mtu mmoja aliyefahamiwa kwa jina la Mohamed Msigara (60) amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea vurugu kati ya wakulima na wafugaji Kijiji cha Dumila, wila yani Kilosa, baada ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima yaliyo katika Kitongoji cha... Mfulu, Kilosa. MAENEO ya mikoa ya Morogoro, Mtwara na Dar es Salaam, jana yaligeuka uwa

King Majuto Anapeta Katika DVD ya Ndoto ya Tamaa

Galacha wa komedi asiye na mpinzani, King Mjuto ameingia taani akiwa na full Package' ya vichekesho ndani ya DVD hiyo inayo kwenda kwa jina  'Ndoto ya Tamaa'. King Majuto kama kawaida yake ndani ya DVD hiyo amefanya balaa la aina yake akiwa ameshirikiana na wasanii nyota kama Nassor Abdi na Jini Msomali. Kampuni inayo husika kusambaza filamu hiyo Pilipili Entertainment inawahakikishia mashabiki wa King Majuto kwamba hakuna atakaye nunua DVD hiyo kisha akajutia fedha                                                                                             zake.     Hii ni Komedi ya ukwelikutoka kwa Mzee  Mjuto ajili ya mwaka 2013 imesema kampuni ya Pilipili.      Tembelea www.pilipilimoviehouse.blogspot.com ilikupata kujua filamu zipi zinatarajia kukita kitaani

Mtazame Beyonce Anavyo 'Shine'

Beyonce Knowles alifanya kitu cha tofauti Washington DC kwa kuingia katika historia ya aina yake kwa kuimba nyimbo ya taifa ya nchi hiyo siku ya sherehe za kuapishwa kwa rais Baraka Obama Beyonce aliongozana na  mumewe Jay Z, siku ya sherehe hiyo.

Dakika ya Mwisho Inamasimulizi ya Ukweli

  Monalisa si Waleo si wakesho MSANII mkongwe katika tasnia ya filamu nchini Yvone Cheryl Monalisa ametajwa kuwa ni miongoni mwa wasanii watakao dumu kwa muda mrefu katika tasnia ya filamu kutokana na wezo walionao. Hayo yamebainishwa baada ya Monalisa  kuonekana  kwa mara nyingine ndani ya filamu inayokwenda kwa jina la Dakika ya Mwisho. Filamu hiyo inazungumzia kijana Masumbuko na Shida  kama watoto wa mtaani wanaoteseka na mazingira ya shida na hatarishi. Kama ilivyo kwa watoto wa mtaani , kwa kuishi na kuomba pamoja Masumbuko(Mkamba)na Shida (Monalisa)wanajikuta wanapendana na kuoana na kuwa Mme na Mke. Wakiwa katika ndoa Shida anapata tatizo la ugonjwa wa tumbo , jambo linaloitaji kufanyiwa upasuaji wa haraka .Lakini tatizo hali zaokiuchumibado ni mbaya. Masumbuko anaangaika kutafuta kiasi cha fedha alicho agizwa na Dokta ilikunusulu maisha ya Mke. lakini akiwa anakabiliwa na mtihani wa kuokoa maisha ya mkewe , Masumbuko anaingia katika janga la kufukuzwa kazi hali inayozidi ku

JK Uso kwa Uso na Blatter

NA MWANDISHI MAALUM, ZURICH RAIS Jakaya Kikwete amelishukuru Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) kwa kuipatia Tanzania misaada mbalimbali ya kifedha na ufundi. Kikwete amesema misaada hiyo si tu kwamba imekuwa ikisaidia kuinua kiwango cha soka nchini, bali pia barani Afrika. Rais Kikwete alitoa shukurani hizo jana baada ya kutembelea makao makuu ya FIFA mjini hapa na kukutana na Rais wa shirikisho hilo, Sepp Blatter. Kikwete aliwasili Zurich akitokea Ufaransa, ambako alifanya ziara ya kiserikali ya siku tatu. Rais Kikwete ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu, ambapo anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa dunia kuhusu uchumi, utakaofanyika katika mji wa Davos. Tanzania ni mwanachama wa FIFA kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). FIFA imekuwa ikitoa dola 250,000 za Marekani kila mwaka kwa nchi wanachama kwa ajili ya kuendeleza soka na dola zingine milioni 2.5 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Shirikisho hilo pia limekuwa likitoa dola 400,000 kila

MAGAZETI YA LEO