Kiongozi wa Umoja wa Afrika na Rais wa Benin Thomas Bon Yayi AFP / Fethi Belaid
Na Lizzy Anneth Masinga
Jumuia ya majeshi ya kijihami ya nchi za Magharibi,NATO imesema kuwa
hakuna mjadala wowote au ombi lolote kwa majeshi hayo kuyasaidia majeshi
ya Afrika Magharibi ili kulichukua eneo la kaskazini mwa Mali
linalodhibitiwa na Waasi wa kiislamu.
Hapo jana Kiongozi wa Umoja wa Afrika, Rais wa Benin Thomas Bon Yayi,
alisema NATO ni budi ikashiriki na Vikosi vya Afrika vikaongoza
Operesheni kama NATO ilivyofanya nchini Afghanistan.
Mali iligawanyika katika sehemu mbili tangu mwanzoni mwa Mwaka jana
baada ya Waasi wa Tuareg kudhibiti miji mbalimbali kaskazini na
Mashariki mwa Mali hatua iliyoleta hofu ya kutoweka kwa hali ya Usalama
katika ukanda mzima.
NATO imesema haijihusishi na Mgogoro hata hivyo wanasikitishwa na hali
ya mambo ilivyo kwa kuwa inatishia hali ya Usalama na utulivu wa nchi
hiyo na katika Ukanda wote.
NATO iliunga mkono Azimio la Umoja wa Mataifa juu ya Mali na uamuzi wa
Umoja wa Ulaya wa kuanza mchakato wa kufunza majeshi yatakayokuwa katika
Operesheni nchini Mali.
Chanzo: kiswahili.rfi.fr.
Comments