Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan akizungumza kwenye mkutano wa Davos |
Na Emmanuel Richard Makundi
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametamka wazi wazi ya kwamba Kundi la
Waislam wenye Msimamo Mkali la Boko Haram ni kitisho kikubwa cha Usalama
katika mataifa mengine ya Afrika na si Taifa lake pekee.
Kiongozi huyo wa Nigeria amekiri vitendo ambavyo vinafanywa na Kundi la
Boko Haram vinadhihirisha waziwazi ya kwamba ni kitisho kwa Wanageria
lakini pia kwa mataifa mengine ya Afrika.
Rais Jonathan amesema eneo la Magharibi mwa Afrika ndilo linaweza
likakabiliwa zaidi na kitisho hicho kutoka kwa Boko Haram kutokana na
kuwa na wapiganaji wanaoongoza mauaji ya kujitoa mhanga.
Jonathan ameweka wazi wamekuwa wakipata taarifa Viongozi wa Boko Haram
wamekuwa wakisafiri na kukutana na Viongozi wa Juu wa Mtandao wa Al
Qaeda Duniani wanaowapatia msaada wa kuendelea na harakati zao.
Boko Haram ni kundi linaloshinikiza serikali ya Nigeria iweze kutambua
utawala wa sharia na kupingana kabisa na mwenendo wa sasa wanaodai
umegubikwa na itikadi za Mataifa ya magharibi.
Via kiswahili.rfi.fr
Comments