Ndugu zangu,
Kule Burkina Faso alitokea kiongozi kijana na mwanamapinduzi. Aliacha hiba njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani.
Aliitwa Kapteni Thomas Sankara.
Mwanamapinduzi huyu kijana alikuja kuawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso.
Sankara alipata kukaririwa akisema;
“Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni, basi, tunastahili ushindi.
Kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu.
Hali hii inatokana na kutoshinikizwa na taratibu zilizozoeleka, kuwa na ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha mustakabali.
Ni wendawazimu wa jana waliotuwezesha kuyafanya tuyafanyao leo.
Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao.”
- Kapteni Thomas Sankara.
Na hilo ni Neno La Leo. Inatoka mjengwa.blogspot.com
Comments