Vijana
wakazi wa Dumila na vitongo vyake wakiangusha gari aina ya Land Cruizer
T 241 AMS mali ya mfugaji katika barabara kuu ya Dodoma-Morogoro wakati
wa vurugu zilizodumu kwa masaa sita kwa kuweka vizuwizi kwa lengo la
kumshinikiza mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bebdera kusikiliza kero za
wakulima.Picha na Juma Mtanda
MWANANCHI
Mkoani
Mororgoro mtu mmoja aliyefahamiwa kwa jina la Mohamed Msigara (60)
amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea vurugu
kati ya wakulima na wafugaji Kijiji cha Dumila, wila yani Kilosa, baada
ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya
wakulima yaliyo katika Kitongoji cha...
Mfulu, Kilosa.
MAENEO
ya mikoa ya Morogoro, Mtwara na Dar es Salaam, jana yaligeuka uwanja wa
fujo na vurugu zilizosababisha vifo, majeruhi na uharibifu wa mali,
huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi.
Vurugu
hizo zimehusisha wakulima na wafugaji wa jamii ya Kimasai kwa upande
mmoja wa Morogoro, Mtwara Mikindani wananchi waliizingira nyumba ya
Diwani wa Kata ya Mikindani kwa madai ya kuwahifadhi watu wanaodaiwa
kuwa washirikina ndani ya nyumba yake, huku Dar es Salaam eneo la
Kariakoo, polisi na Wamachinga wakipambamba na Mgambo wa Jiji.
Mkoani
Mororgoro mtu mmoja aliyefahamiwa kwa jina la Mohamed Msigara (60)
amefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea vurugu
kati ya wakulima na wafugaji Kijiji cha Dumila, wila yani Kilosa, baada
ya wafugaji wa Jamii ya Kimasai kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya
wakulima yaliyo katika Kitongoji cha Mfulu, Kilosa.
Pamoja
na mauaji hayo, wasafiri waliokuwa wakitumia Barabara ya Morogoro –
Dodoma, nao walionja machungu ya vurugu hizo, baada ya kukwama kwa saa 5
kutokana na wananchi wa kijiji hicho, kufunga barabara kwa mawe, magogo
ya miti na kuchoma magurudumu ya gari.
Wananchi
hao walichukua hatua hiyo huku wakisisitiza kutaka kuonana na Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, ili kumaliza mvutano huo.
Katika
vurugu hizo wanakijiji hao walivunja vioo vya madirisha ya baadhi ya
nyumba tano za kulala wageni, kuharibu gari dogo aina ya Landcruser
pamoja na kupora mali mbalimbali zi nazodaiwa kumilikiwa na
wafanyabiashara wa jamii ya Kimasai.
Kabla
ya kufanya uharibifu huo saa 2:30 asubuhi, wananchi hao walifanya
maandamano sambamba na kusimama katikati ya barabara, hali
iliyosababisha polisi kufika eneo hilo kwa ajili ya kuwadhibiti.
Askari
wa Kutuliza Ghasia (FFU), walifika eneo la tukio 5:20 asubuhi na
kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao kwa kutumia mabomu ya machozi,
hatimaye kufungua barabara hiyo.
Pamoja
na barabara hiyo ya Morogoro – Dodoma, wananchi hao pia walifunga
barabara ya Dumila- Kilosa, hivyo kuyafanya magari yaliyokuwa yakitumia
barabara hiyo kukwama kwa zaidi ya saa sita na kusababisha usumbufu kwa
wasafiri waliokuwa wakitumia barabara hiyo.
Wakati
vurugu hizo zikiendelea, wafugaji wa jamii ya Kimasai wakiwamo wanawake
na watoto walionekana kukimbilia kwenye kituo kidogo cha Polisi Dumila
kwa lengo la kujihami na kupata msaada wa polisi kutokana na hofu ya
kushambuliwa na wananchi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo kwenye eneo la tukio, mkulima
aliyefahamika kwa jina Mauya Hamadi alisema kuwa wananchi wamelazimika
kufanya vurugu hizo baada ya wafugaji wa jamii ya Kimasai kuingiza
mifugo kwenye mashamba ambayo tayari yameshapandwa mazao na kufanya
uharibifu.
Alisema
kuwa tayari suala hilo walishalifikisha kwa uongozi wa kijiji, kata,
wilaya hadi mkoa, lakini hakuna jitihada zozote zinazofanywa na
viongozi, hivyo kulazimika kumtaka Mkuu wa Mkoa Joel Bendera, kwenda
kuzungumzia suala hilo, ambapo hata hivyo mkuu huyo wa mkoa hakuwahi
kufika eneo hilo hadi walipoamua kufanya maandamano hayo.
Comments