Na Adnan Hussein, Mogadishu
Serikali ya Somalia itaanzisha mpango mpya hapo Aprili wa kuwalipa
waajiriwa wake kupitia mfumo wa automatiki unaodhibitiwa na Benki Kuu ya
Somalia.
Mfumo mpya katika mwezi wa Aprili utaanza
kutumiwa kuwalipa waajiriwa wa serikali, ikiwa ni pamoja na wajumbe hawa
wa Kikosi cha Polisi ya Somalia, moja kwa moja kupitia Benki Kuu ya
Somalia. [Na AFP Photo/AU-UN IST Photo/Stuart Price]
Waziri wa Fedha na Mipango Mohamud Hassan Suleiman aliiambia Sabahi kuwa
programu hiyo ni moja miongoni mwa mipango kadhaa yenye lengo la
kuufanya mfumo wa fedha nchini kuwa wa kisasa, kutoa uwiano wa bajeti na
kuzuia ufisadi wa kitawala na kifedha.
Waajiriwa wa serikali kwa sasa wanalipwa fedha taslimu na wahasibu
waliopangiwa katika wizara zao husika baada ya fedha kulipwa na Benki
Kuu. Wahasibu ndio wenye dhamana ya kukusanya fedah na kumlipa kila
mwajiriwa baada ya kutia saini risiti ya karatasi kama njia ya
uthibitisho.
Mchakato huu, ambao unahusisha kutoa na kusafirisha kiwango kikubwa cha
fedha na kujaza fomu za karatasi, mara nyingi hupelekea kuchelewa kwa
mishahara na kupotea kwa fedha, Suleiman alisema.
Waziri alisema kuwa mfumo huo mpya utazuia kuchelewa huko na kupelekea
uwajibikaji mzuri zaidi na uwazi katika udhibiti wa fedha za umma.
Kukiwa na mfumo wa malipo ambao ni automatiki, kila mwajiriwa wa umma
atapewa akaunti yake binafsi katika Benki Kuu ambako mishahara yao
itakuwa inawekwa kwenye akaunti hizo na kupatikana kwa kutumia kadi ya
beki mwanzoni mwa kila mwezi.
Comments